Habari

Imewekwa: Feb, 06 2019

Mkurungezi Mkuu TBC asifu ushirikiano mzuri na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

News Images

MKURUGENZI MKUUTBC ASIFUUHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Dr. Ayoub Rioba, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Utangazaji ( TBC), amesifu na kupongeza ushirikiano mzuri anaoupata kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Amesema, uhusiano wa kikazi kati ya Taasisi hizimbili, umekuwana tija katika utekelezaji wa majukumu yaChombo hicho cha Taifacha Habari na kwamba, ni matumaini yake uhusiano huo utaendelea kwa maslahi na maendeleo ya Taifa.

Ameyasema hayosiku ya Jumanne, wakati alipotembeleaBanda la maonesho yaWiki ya Sheria yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere ‘ Square’, Jijini Dodoma

“ Hongereni sana kwa maonesho haya. Miminiwashukuru sana kwa ushirikiano na mahusiano mazuri ambayo tunayo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Hasa katika eneo lamikataba. Sisi kama Chombo chaHabari cha Serikalitunaitegemea sana Ofisi ya MwanasheriaMkuukwa ushauri wa kisheria naupitiaji wa mikatabayetu ya kibiashara” akasema Mkurugenzi Rioba

Na kuongeza “Kwa mazingira yakazi zetu, na hasa paletunapohitaji kununua vifaa au mitambo yaradio au televisheni nilazima tulete mikataba yetu kwenu ili iweze kupatiwa ushauri wa kisheria.Kwa hiyo upitiaji wa mikatabayetu na kutolewa kwa wakati ni jambo lenye tija kwetu na katika utekelezaji wa majukumu yetu kwa maneno mengine sisi ni wadau wenu”.

Akatoa mfano kwa kusema pala kifaa kinapo haribika labda kwa kupigwa na radi ni wazi kwamba mchakato wa kukinunuaukiwamomkatabalazima ufanyike nauhusishe Ofisi yenu, nauharaka wa ununuzi wa kifaa hicho na kwa kuwa radio au televisheni haiwezi kutokuwapo hewani kwa mudamrefu ndiyo maana kutokana unyeti huohatamchakato wake unabidi uwe waharaka lakini kwa kuzingatia matakwa ya kisheria.

Mawakili wa Serikali, Obadia Kajungu na Anna Mkongwa waliokuwa wakitoa huduma za ushauri kwa wageni waliokuwa wakifika katika Banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, walimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TBCkwa kufika katika bandahilo.

“Tunakushukuru kwamba unaridhishwa na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo baina yetu. Ushauriulioutoa hasa waupitiaji wa mikataba na kuitoa kwa wakati tutauzingatia na kuufishangazi za juu. Tukushukuru pia kwa kututembelea katika banda letu na kujielimisha kuhusu majukumuna utendaji kazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu” akasema WakiliObadia Kajungu.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikaliikiwa niMdau wa Mahakama ilishiriki maonesho hayoyaliyoanzaJanuari 31 na kukamilika FebruariTano. Huduma zilizotolewa na Mawakili wa Serikali kwawageni waliofikakwa shindambalimba ni pamoja na, kutoa ushauri wa kisheria, kujibu na kutoa ufafanuzi kuhusu changamoto za kisheria ambazo baadhi ya wageni walikuwa nazo, kuelezea nakufafanuanafasiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ujumla.

Baadhi yawageni walielekezwa wapi auTaasisigani wanapashwa kwendakupata msaada ziadi wa shida zao.

Pia Mawakili wa Serikalihao walitoahuduma ya uelimishaji kwa wanafunzi wa sekondari na Vyuo Vikuu waliofikaau kupangiwa katika banda la Mwanasheria Mkuu ikiwa ni sehemu ya mfunzo .