Habari

Imewekwa: Dec, 13 2018

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali afungua kikao kazi kujadili Mpango Mkakati wa Ofisi

News Images

WADAU WAJADILIMPANGO MKAKATI WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Na Mwandishi Maalum- Dodoma

Mabadiliko yaMuundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yataiwezeshaOfisi hiyo, kuimarisha weledi na ubobezi wa kitaalamu katika kuishauri Serikali katika masualayote ya kisheri. Hususani katika kipindi hiki ambacho Serikali imejielekeza katika uchumi wa viwanda na uchumi wa kati.

Hayoyameelezwa leo alhamis naNaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa wakati akifungua mkutano na Wadau wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwaajili ya kupitia rasimu ya Mpango Mkakati mpya wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Majadilianohayo yamefanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Hifadhi yaChakula JijiniDodoma na kuwashirikisha wadau kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali zaidi ya 15 ambazo kwa namna moja ama nyingine wanafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Naibu Mwanasheria Mkuu amewaelezawadau hao kwamba, Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali imeandaa rasimu ya Mpango Mkakati wamiaka mitano kuanziamwaka 2019/20-2023/24 kutokana na mabadiliko yaMuundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu yaliyofanyika kupitia tangazo la Serikali Na. 48 na piakuisha kwa muda wake Mkakati wa mwaka 2012/2013-2017/2018

" Wadau wetu,rasimu ya Mpango Mkakati huu ambao tunaiwasilisha kwenu kwajili ya kupata maoni yenupamoja na kuuboresha, Umezingatia Sera,Mikakati na Miongozo Mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa". Akasema.

Na kuitajabaadhi ya mipango hiyo kuwa ni, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania-2015, Mpango wa Pili wa Taifa wa Miaka Mitano, Malengo yaliyopo kwenye Ilani ya Chama Tawala ya mwaka 2015 na Malengo ya Maendeleo Endelevu yaUmoja wa Mataifa (DSGs ).

Dkt. Longopa, amewahimiza wadauhao kutoa maoni yao , ushauri na waeleze niyapi matarajioyao kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akizungumziazaidi kuhusu rasimu hiyo , Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amebainishakwamba, Mpango Mkakati huo pia umeainisha hali halisi ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yakiwao majukumu, mafanikio mbalimbali ya kiutekelezaji yaliyopatikana, uchambuzi wa Ofisi kwa kutumia mfumo " SWOT Analysis", Changamoto zilizojitokeza pamoja na maeneomuhimu yatakayo jumuishwa katika Mpango Mkakati wa mwaka 2019/20-2013/24.

Dkt. Longopa amezitaja nguzo kuu tatu ambazo kupitia Mpango Mkakati huo zitasimamiwa katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi.Nguzo hizo niHuduma bora za Kisheria,Kufanya Maboresho ya Mifumo ya Taasisi na Uhamasishajina Usimamizi waRasilimali.

Akimkaribisha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuzinduamajadiliano hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Bibi Nkuvililwa Simkanga, amesema,Rasimu ya Mpango Mkakati wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaliwa namaafisa kutokaIdara ya Mipango pasipo kutegemea wataalamu kutoka nje ya Ofisi.

Akasisitiza kuwa, Mafunzo ambayomaafisa wa Idara ya Mipangowamepewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yamewajengea uwezomkubwakiasi ambacho wamefanikisha kwa weledi mkubwa kuandaa rasimu hiyo na ambayo sasa inawasilishwa kwa wadau kwa maoni na ushauri wao.

Akitoamaoni ya jumla, mdau kutoka Sekta ya Uchukuzi Bw. Paulo Laizer amewapongeza watalaam wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuanda rasmu bila yakutumia wataalamu kutoka nje.

"Niwapongeze kwa hatua hii muhimu sana, sasa inaonyesha tunakokwenda, uamuzi huu wa kutumia wataalamu wenu si tu unathihirishanamna mlivyotumia vema mafunzo ya uwezeshwaji mliyopewa nawataalamu wa Ofisi ya RaisMenejimenti ya Utumishi wa Umma naUtawalaBora, lakini piauamuzi huoumeokoa fedha ambazo zingetumika kuwalipa wataalamu wa nje.