Habari

Imewekwa: Dec, 13 2018

WADAU WAJADILI RASIMU YA MPANGO MKAKATI WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

News Images

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewasilisha mbele ya wadau wake rasimu ya Mpango Mkakati wake wa mwaka 2019/2020-2023/2024. Mpango huo umewasilishwa kwa wadau ili waweze kutoa maoni yao ikiwa ni pamoja na kuangalia namna bora ya kuuboresha ili hatimaye uweze kuisaidia Ofisi katika utekelezaji wa jukumu lake la kuishauri Serikali katika masuala yote yanayohusu sheria.