Habari

Imewekwa: Feb, 08 2019

Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wapanda miti

News Images

WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWAKUTUNZA MITI WALIYOIPANDA

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Naibu Mwanasheria Mkuu wa SerikaliDr. Evaristo Longopa amewatakawatumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakisha kwamba,mitiwaliyoipanda leo inatunzwa ipasavyo na kukua ili ipendezeshe mandhari ya Ofisi na kuhifadhi mazingira.

Dr.Longopa ametoa wito huo leo, Ijumaa, wakati alipowaongoza watumishi wa Ofisi yake katika zoezi la upandaji miti, katikakiwanjainapojengwa Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali katikaMji wa Serikalihuko Ihumwanje kidogo ya Jiji la Dodoma.

Mitiambayo imepandwa katika zoezi hiloni 75kati ya 640 inayotarajiwa kupandwa katika eneo hilo. Miti hiyo 75 ni aina yaAshoki naMiti Maji au maarufu kama miti Dodomaimepandwa kama sehemu yampaka wa kiwanja cha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Watumishi wenzangu, leo tunazinduazoezi la kupanda miti 75 kati ya640ikiwamo ya matunda ambayo tutapanda katika eneo letu.Upandajihuu wa mitiunayo malengo tuseme mawili, kwanza kupendezesha mandhari ya eneo la Ofisi yetu ili yawe ya kuvutia na pili ni kuhifadhi mazingira.Niwatake basi tusiishie kupanda tu bali kila mmoja wetu ahakikishe anatunza miti hii iliiweze kukua na kustawi”. Akasema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu kuongoza na kushiriki zoezi hilo, wangine walioshiriki nipamoja na Mkurugenzi wa Mipango Bi. Nkuvililwa Simkanga na Bw. Jackson Nyamihula ambaye n Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu.

Kwa upande wao watumishi hao wakionesha kufurahia zoezi hilola upandajimiti, baadhi walipendekeza kwambakila aliyepandamtu aweke alama yake ilikuhakikisha kwamba kila mmoja anautunza mti wake.

Baada ya zoezi la upandajimiti, Naibu Mwanasheria Mkuualikwenda kukaguamaendeleo yaujenzi wa jengo la Ofisi ambapo mmoja wa ma – Injinia anayesimamiaujenzi huo Injinia Suma Atupele alimweleza Naibu Mwanasheria Mkuu kwambakazi inaendeleavizuri ambapo kazi mbalimbali zikwamo za uchapiaji na upakaji rangi na nyinginezo nyingi zimekuwa zikiendelea kwa kasi ya kuridhisha.