Habari

Imewekwa: Jun, 19 2020

Na Mwandishi wetu, Dodoma

News Images

AG AFANYA MAJADILIANO NA UONGOZI WA TLS

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi, jana ( jumatano)amekuwa na kikao cha kisheria na Kamati yaUendeshaji ya Chama cha Wanasheriawa Tanganyika(TLS).

Kwa mujibu wa Mwandishi Mkuu wa SheriaBw. OnoriusNjole ambaye alishiriki kikao hicho, amesema, katika kikao hicho cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali naBaraza la Uendshaji la TLS walijadiliana na kufanya mashauriano kuhusu kutungwa kwa Kanuni mbalimmbali zaChama hicho.

Akifafanua zaidi, Bw. Njole amebainisha kwamba,kikao hichocha kisheria, kimefanyika kwa mujibu wa kifungucha 31 cha Sheria ya Chama cha Mawakili ambacho kinaitaka TLS inapotunga kanuni zozote kufanya mashauriano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Baraza la Uendeshaji la TLs liliongozwa na Rais wa Chamahicho Bw. Rugemeleza Nshala.