Habari

Imewekwa: Oct, 07 2021

AG AHIMIZA USHIRIKIANO JUMUISHI WA TAASISI TATU

News Images

AG AHIMIZA USHIRIKIANOJUMUISHI WA TAASISITATU

Na Mwandishi Maalum

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshi, amesitiza kwamba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa yaMashtaka zinabeba Taswira ya Nchi, na hivyo kuzitaka Taasisi hizo kufanyakazi kamatimu moja.

Ameyasema hayo katika mkutano wakeuliowajumuisha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt Boniphace Luhende, Kaimu Naibu Mwendesha Mashtaka Neema Mwenda, na Wakurugenzi wa Idaraza Mipango za Taasisi hizo tatu.

Mkutano huo umefanyika leo Jumatano, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mtumba, Jijini Dodoma.

“ Taasisi hizi zinabeba taswira ya nchi, rai yangukwenu ningependa kuonatunafanya kazi kama timu moja, tunakuwa na ushirikianojumuishi bila ya kuathiri majukumulengwa ya Kitaasisi kwa mujibu wa miundo ya Taasisi, kwa sababu wote tunaitumika Serikali moja, Serikaliambayo ipo tayari kutusaidia katika utekelezaji wa Majukumuyetu”. Amesema Dkt. Feleshi.

Na kwa sababi hiyo, akasema, ndiyo maana ameamua kuitisha kikao hicho ambacho pamoja na mambo mengine, amewapa watendaji wa Taasisi hizo, jukumu la kuandaa mchanganuona mapendekezo ya kinaya maeneo ambayoyatajengewa hoja za kuomba kuongezewa bajeti katikamwaka wa fedha 2022/2023.

Dkt. Feleshi amebainisha kuwa, ikiwa ni miaka minne (4) sasa tangumaboresho ya mwisho yaliyofanywa na Serikali mwaka 2018, maboresho yaliyopelekea kuundwa kwa Taasisi hizo tatu ili kuongeza ufanisikatika utekelezaji wa majukumu . Badolengo lamaboresho hayo, halijaweza kufikiwa kutokana na Taasisi hizo kukabiliwa na changamoto mbalimbali likiwamo hilola ufinyu wa bajeti.

Akasema ameshakutana nakufanya mazungumzokwanyakati tofautinaMwendesha Mshtaka Mkuu, na Wakili Mkuu wa Serikali na katika mazungumzoyao yapo mambo ambayo wamekubaliana kuyafanyia kazi.

“Nipo katika kujifunza, leonimewaita nyinyikwa sababu ndiyo maafisa masuhuliili kwapamojatujadiliane na kubadilishana mawazo ya namnaTaasisi hizitatu zitawezakuandaa bajeti zenye uhalisia na zinazozumza kulingana na ukubwa wa majukumuyetu na changamototunazokabiliana nazo ”. Akasema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Amesisitiza kwamba, kilaTaasisiiandae mchanganuo wake na mapendekezo kwa kuzingatiavipaumbele vyake muhimu na ambavyoni halisia. “Kunamambo mengine lazima tufanyepamoja na hii ndiyodhamirayangu, lakini kama miongoni mwenu yupoanayetaka kwenda peke yake sawa tu, lakini nadhani tukienda pamojatutakuwa na tija zaidi.

Hata hivyo amekiri kwamba,Serikali haiwezi kufanya kila kinachoombwa katika bajeti inayoombwa na Taasisi, lakini kubwa na la muhimuni kuandaa bajeti yenye uhalisia na zitakazoifanyaTaasisi hizo kuendesha shughuli zake kwa weledi na kwa kuzingatia hadhi na taswira ya nchi.

Pamoja nachangamoto kubwa ya ufinyu wa BajetiunaozikabiliTaasisi hizo tatu, pia zinakabiliwa na upungufu mkubwawa watumishi hususanimawakili wa serikali na wa kada nyingi. Kwa upande wa mawakili wa serikali peke yake kuna upungufu wa mawakilizaidi ya 4,303 katika Taasisi zote tatu.

Viongozi waliohudhuriakikao hicho wamemshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikalikwa kuitisha kikao hichomuhimu ambapo pia kimeweza kuwapatia fursa ya kufahamu maonoyake, vipaumbele vyake na mwelekeo wa mbeleni wa Taasisi hizo. Na kuahidi kwamba, watakwenda kuyafanyikakazi maagizo na maelekezo yake kwa wakati.