Habari

Imewekwa: Oct, 06 2021

AG AHUDHURIA UZINDUZI WA VITUO JUMUISHI

News Images

AG AHUDHURIAUZINDUZI WA VITUO JUMUISHI

Na Mwandishi Wetu

Dodoma

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshileo, (jumatano) ameungana naviongozimbalimbali katika haflamaalum yauzinduzi waVituo Jumuishi Sita vya Utoaji wa Haki Nchini.

Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiye aliyefanyauzinduzi huo kwa kuzindua Jengo la Kituo Jumuishi cha UtoajiHaki katika Jiji la Dodoma. Jengo hilo la kisasa lipo katika Mtaa wa NCC nyuma yaJengo la Benki Kuu.

Uzinduzi wa Jengo hilo laDodoma, umewakilishamajengo mengine yaliyojengwa katikamikoa ya Arusha , Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam.

Majengo yote sita yamegharimukiasi cha shilingiBilioni51.5 ambao ni mkopo kutoka Banki ya Dunia.

Majengo hayo pamoja na mambo mengine,yatakuwa na mahakamaya watoto,mahakama yaMwanzo,mahakamaWilaya , mahakama ya Hakimu Mkazi,Mahakama Kuu na Mahakamaya Rufaa. Na kuna eneo maalum ambalo limetengwa kwaajili yaMahakimu naMajaji

Vile vile majengo hayo ambayoyana milango mitano ya kuingilia, piayana sehemu maalumu ambayo itawapa fursaakina mamakunyonyesha watoto wao kwa faragha.

Majengo hayo piayana vyumba ambavyo vimetengwa kwa ajili yawadau mbalimbali wa Mahakama wakiwamo Mawakili wa Serikali,Waendesha Mashtaka,Mawakili, Polisi, Magereza na Ustawi wa Jamii.

Muundo au ramani yamajengo haya kutawafanya wananchi wanaokweda hapo kupata huduma zote katikaJengo moja na hivyo kupunguza gharama na muda.