AG FELESHI AKUTANA NA BALOZI WA SINGAPORE

Imewekwa: 30 Aug, 2022
AG FELESHI AKUTANA NA BALOZI WA SINGAPORE

Na Mwandishi Wetu

Mwanasheria Mkuu wa  Serikali  Jaji Dk. Eliezer Feleshi jana  jumatatu amekutana na kufanya mazungumzo na  Balozi wa Singapore nchini Tanzania Mh. Douglas FOO.

Balozi Douglas FOO mwenye  makazi yake Nchini Singapore alifika Ofisini kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma kwa  lengo la kujitambulisha.

Pamoja na  kujitambulisha  viongozi hao wawili  walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano   kati ya nchi hizi mbili.

Hii ni  mara ya kwanza kwa Balozi  Douglas FOO kukutana na Mwanasheria  Mkuu wa Serikali.

Balozi  huyo  wa Singapore  yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo amekuwa akikutana na viongozi  mbalimbali wa Serikali.

Nchi ya Singapore inamahusiano ya  kidiplomasia na nchi 150 duniani Tanzania ikiwamo.

30 Agosti 2022