Habari

Imewekwa: Nov, 12 2021

AG FELESHI AMSHUKURU RAIS SAMIA

News Images

AG FELESHI AMSHUKURU RAIS SAMIA SULUHU

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

MwanasheriaMkuu wa Serikali (AG)Dkt Eliezer Feleshi amemshukuruMhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwakumuamini na kumteua katika nafasi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali.

Dkt Feleshi ametoa shukrani hizo leo( Alhamisi) JijiniDodoma, akisimama kwamara ya kwanza mbele yaBunge hilotangu alipoteuliwa kuwa AG na baada ya kula kuiapo cha uaminifu kwa Bunge hilo, wakati alipokuwa akiwasilishaMuswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ( Na 6) wa mwaka 2021 katika Mkutano wa Tano waBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Napendakuchukua fursa hii kumshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania kwa kuniamini nakuniteuakatika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.” AkasemaAG Feleshi

Na kuongeza “ Ninamuahidi kutekelezamajukumu yangu haya mapya kwa weledi,umahiri na uamininifu mkubwa”.

“Pili nimshukuru Mungu tena kwa kuniwezesha kusimamakwa mara ya kwamba mbele yaBunge lako Tukufu kuwasilisha Muswada waMarekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Na 6) wa Mwaka 2021” akasemaMhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akiwasilisha Muswada huo wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Na 6)wa mwaka 2021 ( The Written Laws ( Miscelaneous Amendiments) No (6), Bill.2021, MwanasheriaMkuu wa Serikali amesemaMuswada huo unapendekeza marekebisho katika sheriazifuatazao;

Sheria yaKodi ya Mapato, Sura ya 332; Sheria yaUsimamizi wa Kodi, Sura ya 438 na Sheria yaKodi la Ongezeko la Thamani, Sura ya 148.

Kwa mujibu wa AG Feleshi, Muswada aliouwalisha mbele ya Bunge, umegawanyika katika sehemu Nne ambapo sehemu ya kwanza ya Muswada inaainisha masharti yautagulizi, ikiwa ni pamoja na jina la Sheria pendekezwa na tamko la marekebisho ya sheria mbalimbali zinazokusudiwa kufanyiwa marekebisho kupitiaMuswada huo.

Akalieleza Bunge hilo kwamba,sehemu ya pili ya Muswada huo inapendekeza marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya332, ambapokifungu cha 83Bkinapendekeza kufutwa kwa lengo la kuondoa kodi yazuioya asilimia mbili kwa mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.

“Lengo la marekebisho ya haya nikulinda vipato vya wakulima kwa kuwapunguzia mzigo unaotokana na utozwaji wa kodi” amebainisha Dkt. Feleshi.

Kuhusu sehemu ya tatu ya Muswada, ikisomwa pamoja na Jedwali la marekebishoa yaSerikali , inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Usimamizi wa kodi Sura ya 438 ili kurekebisha kifungu cha 7 kwakuongeza kufungu kidogo cha 3.

“Marekebisho hayoyanalenga kutambua Mkataba wa utekelezaji waMradi wa Bomba lakusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Chongoleani Tanga ili utekelezaji wa sheriaza kodi usiathiri masharti mahususi ya mkataba huo kama ilivyokubaliwa na pande zote

Kuhususehemu ya Nne ya Muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema,upande wa sehemu ya Nne yaMuswada inayopendekeza marekebisho ya kufutasheria ya kodi ya ongezeko la thamani Sura ya 148, inapendeleza kufutwa. “ Hatua hiyo inatokana namashauriano yakinakati yaSerikali na Kamati

WAKATI HUO HU, Mwanasheria Mkuu wa SerikaliDkt. Feleshi, amewapongeza watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt, Evaristo Longopa kwa kuendelea kutekeleza majukumu nakazi za Ofisiya MwanasheriaMkuu wa Serikali, ikiwamo kuandaa Muswada huo na ambao umesimamiwa kwa karibuna Bw, Onorius Njole, Mwandishi Mkuuwa Sheria akishirikiana na Waandishi wa Sheria wa Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali.

“ Tunatambua na tutaendelea kutekelezamajukumu yetu kwaweledi, ufanisi nakuweka mbele maslahi ya nchi yetu” amesisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Feleshi.

Imetolewa naKitengo cha Mawasiliano

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

11/11/2021