Habari

Imewekwa: Nov, 24 2021

AG FELESHI AWATAKA WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO KUWEKA MALENGO YA KAZI

News Images

AG FELESHI AWATAKA WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO KUWEKA MALENGO YA KAZI

  • Atilia mkazo uadilifukazini
  • Asema Maslahi ya Watumishiyataboreshwa
  • Atiliamkazoulipaji wa madai na stahiki za watumishi
  • Ataka mafunzo kazini kutiliwa mkazo
  • Awataka Watumishi wote kuishi kama familia moja

Na Mwandishi Maalum

Mwanza

Wakuu wa Idara na Vitengokatika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wametakiwa kuweka malengopamoja na kuwa namiongozo ya ndani itakayoainisha shabaha na muda wa kutekeleza kila kazi.

Ametoa wito huo katika siku ya kwanza ya mkutano wa siku mbili wa Baraza la Wafanyakazi laOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaofanyikaJijini Mwanza.

Dkt. Feleshi amesema, Kupitia kikaohicho cha Baraza angependakukitumia kukumbushana mambo machache kuhusu utendaji kazi wetuwa kila siku katikamaeneo kadhaa.

Eneo la kwanza ambaloMwanasheria Mkuuamewakumbusha wakuu hao wa Divisheni na Vitengona watumishi wote wa ujumla,ni kuhusu majukumu yetu ya kazi ambapoamesisitiza kwamba ni wajibu wa kila mtumishi kuzitambua na kuzianisha kazi,kuzielewa na kuzitekeleza kwa weledi.

Kwa mujibu wa MwanasheriaMkuu wa Serikali anasema Uzoefu unaonyesha kuwa watumishi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea.

Eneo la pili ambaloDkt. Feleshiamelikumbusha ni kwa wakuu Divisheni na Vitengo kuweka malengo ya kazi.

“Ninatoawito kwa Wakuu waDivisheni na Vitengo kuweka malengo, kuwa na miongozo ya ndani kwa kuanisha shabaha na muda wa kutekeleza kila kazi kwa ufanisi na kwa wakati.” Amesisitiza Dkt. Feleshi.

Aidha amebainishakuwa , Wakuu wa Divisheni na Vitengo wanatakiwa kuhakikisha uwepo wa mambo matatu wakati wa kutekeleza mpango kazi wa Ofisi.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni; kueleweka kwamajukumu ( clarity), kwamba kiongoziahakikishe kazi inayotolewamaelekezo na aliyempa kufanya kazi hiyo anaelewa nini anatakiwakufanya.

Jambo la piliambalo ameelekeza kwa wakuu wa divisheni navitengo kuzingatia ni; uwezo au umahiri( competence) kwamba, mtumishi anayepewa kazi anao uwezo wa kuielewa na kuitekeleza kazi hiyo kwa ukamilifu pasipo makosa.

“Jambo la tatu ni mazingira wezeshi ( Climate) kwamba, pawepo na mazingira wezeshi na yenye kumwezesha mtumishi kufanya kazi zake kwa ufasaha na kufikia malengo yaliyokusudiwa hii ni pamoja na kuwepo kwa vitendea kazi” amebainisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eneo laTatu ambaloamewakumbusha Wakuu waDivisheni na Vitengo pamoja na watumishi wote nisuala la uadilifu ambapopamoja na kutilia mkazokuzingatia maadili ya utumishi wa umma, lakiniamehimiza kutumiwa kwa njiaya kuelimishana na kuchuka hatua stahiki mapema kwa watumishi wenye viashiria vyakutekeleza majukumu yao kinyume na maadili.

“Ofisi iwe ni sehemu ya malezi na siyo kusubiri kutibu tatizo, aidha uzingatiaji wa uadilifu tuuhimize pia kwa Taasisi ambazo ni wadau wetu wa ndani ya nje ambao tunafanya nao kazi” akasema.

Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amesisitiza haja na umuhimu wa kujenga uwazi katika mifumo yetu ya kutekeleza majukumu na vilevile kuomba mrejesho kutoka kwa wadau.

Kuhusu Maslahi ya Watumishi, Mwanasheria Mkuu wa Serikaliameeleza kwamba, amekwisha kutoa maelekezo kwa Menejimentiya Ofisikuandaa andiko la kujenga hoja ili Bajeti ya Ofisiyetu na Taasisi zake ziweze kuongezwa nakuwezesha kutatua changamoto zilizopo katikamaeneo ya ununuzi wa vitendea kazi, kuboresha maslahi kwa watumishi na mafunzokwa watumishi.

“Hivyo natoa wito kwa Idara zinazohusika na kazi hiyo kukamilisha kazi hiyo ambayo pia iliridhiwa na kikao cha ( Government Legal Team) kilichofanyika Novemba 22, 2021 ili tuweze kuwasilisha andiko hilo kwenye mamlaka husika” amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akielezea zaidi kuhusumaslahi ya watumishi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa na haya ya kusema

“Kulingana nahali ya kifedha tunayopokea katika Ofisi, hatuna budi tuendelee kutoa kipaumbelekulipa stahiki za watumishi, kwani kwa kulipa madai na stahiki zao mbalimbali kwa wakati tutakuwa tunatekeleza matakwa ya kisheria”

Katikasiku ya kwanza ya Baraza , wajumbe walipata nafasi ya kupokea taarifa mbalimbalina kisha kuzijadili na pia kutolewa ufafanuzi Makamu Mwenyekiti wa BarazaNaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Longopa na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo naWasimamizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalikutoka mikoa Tisa ambako Ofisi hizo zipo.