Habari

Imewekwa: Sep, 13 2021

AG FELESHI AWATAKA WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUJITHAMINI

News Images

AG FELESHI AWATAKA WATUMISHI KUJIAMINI, KUJITHAMINI

Na Mwandishi wetu

Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt.Eliezer Mbuki Feleshiamesema, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalini Ofisikubwa na inayotegemewa, kwa sababu hiyo, amewatakawatumishi wa Ofisi hiyo kujiamini na kujithamini.

Ameyasema hayo leo wakati wa kikaochake kifupi na Mejimenti ya Ofisiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ikiwa ni muda mfupi tangu kuapishwa kwake na Mhe. Rais Samia Hassan Suluhu kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kabla ya kuzungumza naMenejimenti, na akiwa ameongozana naNaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa, Dkt. Feleshi alipokelewa kwa shangwe na bashasha kutoka kwa Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliokuwa wamejipanga nje yaOfisi hiyo ambapo pia walimkabidhiMaua naKadi ya pongezi kwakuteuliwa kwake

“Hii ni Ofisiinayotegemewa, watumishi wanatakiwa kujithamini ilikwa uchache wetu, au kwa uwingi wetu tufanye kazi kama timu, tuyaendeleze yale ambayoyanapashwakuendelea kufanyiwa kazi au yale ambayo yamefashafanyiwa kazi na kuwa tayari wakati wowote.

Ameelezea kuridhishwa kwake nautekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kwamba amekuwa akifuatilia kwa karibu,

Amesema, amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 27 miaka ambayopia na alifanya kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kwamba, hakutegema kamaangerudi tena katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Amesisitiza kwa kusema, maisha ya kila mtu ya kila siku niya kujifunza, hakuna mtu anayeweza kusemaanajua kila kitu, wala hakuna mtu anayeweza kuanzisha kitu na kukikamilisha mwenyewe bila ya kumtegemea mwingine. “ Na ukishaapishwa mzigo wote unakuwajuu ya mabega yako. Miminikuku mwenye kambamguuninipo tayari kujifunza kutoka kwenu”.

Kwa upande wao,Menejimenti hiyoikiongozwa naNaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, pamoja na kumkaribisha wamemuahidi kumpatia ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu aliyokabidhiwa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Eliezer Feleshi anakuwaMwanasheria Mkuu wa Serikali wa kumi (10) tangu kuanzishwa kwa Ofisi hii.