Habari

Imewekwa: Nov, 14 2019

AG KILANGI ATETA NA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

News Images

AG PROFESA KILANGI ATETA NA TUME YAHAKI ZABINADAMU NA UTAWALA BORA

DODOMA , Nov 13,2019

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi( AG)leo ( jumatano) amekutana na kisha kuwa na mazungumzo naUjumbe waTume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Mazungumzo baina ya AG na Tume hiyo ambayo iliongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Mhe. Methew Mwaimu yamefanyika katika Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali iliyopo katika Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Jaji Mstaafu Methew Mwaimu alimueleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwamba, Madhumuni ya ziara hiyo pamoja na masuala mengine, yalikuwa ni kujitambulisha kwake lakini piakujadiliana nakubadilishanamawazo ya namna Ofisi hizo mbili zinaweza kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa majukumuyao.

Kwa upande wake Profesa Kilangi, aliishukuru Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala bora wa kuona umuhimu wa kumtembeleanakubadilishana naye mawazoikiwa ni muda mfupi tangukuteuliwa kwao na kuapishwa kwao.

AG ameiahahidi tume hiyo ushirikiano madhubuti kutoka katika Ofisi yake.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu na Huduma za Kisheria, Dkt. Gift Kweka.

Itakumbukwa kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Jaji Mstaafu Methew Mwaimu na Makamisha wake waliteuliwaMwezi Septemba mwaka huu naMhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.