Habari

Imewekwa: Nov, 06 2019

Badirikeni au Jamii iwabadirishe- AG

News Images

BADIRIKENI AU JAMII IWABADIRISHE-AG KILANGI

Na Mwandishi Maalum,

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus KilangiamewaasaWanasheria wa Serikali katika Utumishi wa Umma kukubali mabadiliko, kubadilika na kujibadili vinginevyo jamii itawabadili.

Ameyasema hayo jana ( alhamisi) jijini Dodoma, wakati akihitimishakikao kazi cha siku mbili baina yake naWakurugenzi wa Sheria na Wakuu wa Vitengo vya huduma za kisheria kutoka Wizara,Mashirika, Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Taasisi mbalimbali za serikali.

"Tumekutana hapa kwa siku mbili, tumejadiliana mafanikio na changamoto zinazotukabili katika taaluma yetu, tumebadilishana mawazo ili sote tuwe na picha ya pamoja, niwashukuru kwa michango yenu, mawazo yenu na na mapendekezo yenu sura moja na na lengo letu ni moja tu tunajenga nyumba moja ambayo ni serikali ambayo mwisho wa siku tuijengee nchi yetu na watu wake na hii nchi inamatarajio yake, inamatumaini yake na sisi ni sehemu ya mchakatao huo"

"Lakininisemekwa namna moja ama nyingine picha ya wanasheria katikajamii siyo nzuri sana, tunaweza kuwazungumzia mawakili wa kujitegemea lakini pia wanasheria wa serikali wamo katika mkumbo huo " amesema Mwanasheria Mkuu.

Na kwa sababu hiyo akawataka wanasheria hao wa Serikali kwamba wanalazimika kubadirika."tusipobarilika tutabadirishwa na jamii, tutabadirishwa na mazingira na hii ni kwa wanasheria wote hata mawakili wa kujitegemea"

Profesa Kilangi akabainisha kwa kusema"mtu wa mtaani anaangalia namnagani haki inatendeka, namna ganimambo yanayomgusa katika maisha yake yanathaminiwa na kutekelezwa kwa misingi ya haki, haangalii mbwembwe zako au lugha unayoongea hayo hayamhusuanataka haki itendeke kwa hiyo kubadirika ni lazima, kujibadilisha ni wajibu na lakini ili ufanye mabadiriko yatakayokuacha salama lazima ujitengenezee utaratibuunataka ubadirike vipi na kwa namnma gani na ndiyo sababu ya kukutana hapa kwasiku mbili"

Amewaeleza Wanasheria hao katika utumishi wa umma kwambaserikalina nchi kwa ujumla imo katika mabadiliko makubwa. " Na sisi ni sehemu ya mchakato huo wa kuijenga nchi na hasa kushughulikiamatatizo ya watu katika eneo hili la sheria".

Akizungumziazaidi kuhusu mabadiriko, Profesa kilangi amesema, mabadiliko huambatana nawasiwasi na taharuki na kwamba hata miongoni mwa wanasheria hao wa serikali wapowenye wasiwasi lakini akawahakikishia kwamba mabadiriko hayo hayalengi katika kumkomoa mtu bali ni katika kuboresha utekelezaji wa majukumu yao na kuwajengea mazingira bora zaidi kamaWanasheria wa Serikali.

Akizungumza kwa niaba yawashiriki wa kikao kazi hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara yaHuduma za Sheria Ofisi ya Rais- TAMISEMI Bw. Eustard Ngatale amemshukurua Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuandaa kikao kazi hicho na kuomba Miongozo mbalimbaliiliyowasilishwa kwao ikamilike haraka ili waweze kuitumia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Rasimu yaMiongozo iliyowasilishwa kwaWanasheria hao ni Muongozo wa kutunga sheria ndogo;Muongozo ya upekuzi wa Mikataba mbalimbali;Muongozo wa majadilianoya Mikataba yote;Muongozo wa usimamizi wa utekelezaji wa Mikataba na Muongozo wa utoaji wa ushauri wa kisheria.

Vile vile katika kikao kazi hiki wanasheria wa Serikali walisitizwa kuhakikisha kwamba hukumu zinazotolewa na mahakama baada ya kesi kumalizika zinatekelezwa ili kuepuka matatizo yanayotokana nakutotekelezwa kwa hukumu hizo.

Bw.Ngatala amesemaKikao kazihicho baina yao na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kimewapa matumaini nafaraja kubwa kwamba sasa wanamahali pakuzungumzia mafaniko na changamoto wanazokabiliana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Vile vile kwa niaba ya washiriki, Bw Ngatala wamekubaliana na hoja ya kubadilikakatika utekelezaji wa majukumi yao nakwenda kusimamiataaluma yao.

Wanasheria hao wamependekeza vikao kazihivi kufanyika mara kwa marakwa lengo la kuelimishana na kuweka sawa katika kuhakikisha kwamba wanatekeleza majukumu yao kwa welendi na tija.

mwisho