Habari

Imewekwa: Sep, 05 2019

KAMATI YA UKAGUZI WA NDANI YASISITIZA UREJESHWAJI WA MASURUFU

News Images

KAMATI YA UKAGUZI YASISITIZA UREJESHWAJI WA MASURUFU

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Kamati yaUkaguzi ya Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali, imeiagiza Idara ya Uhasibu kuhakikisha kuwa, inaendelea kusimamiasuala ya urejeshwaji wa masurufu kwa wakati kwa kila anayepaswa kufanya hivyo.

Agizo hilolimetolewa leo (alhamisi)wakati Kamati yaUkaguzi ilipokutana katika kikao chake kilichopokea na kujadilitaarifa za Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kikao hicho kimefanyikakatika ukumbi wa mikutano waOfisi ya Ipagala.

Bw. Costantine Mashoko kutoka Wizara yaFedha na Mipango na ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo amesema, wakati wanampongeza Mhasibu Mkuukwa kulisimamia vema suala hili,na vilevile kwa kuanza mwaka mpya wa fedha bila kuwa na madeni makubwa yaurejeshwaji wa masurufu, usimamizi huo unapashwa kuwa endelevu.

Pamoja na pongezi hizo, Bw.Mashoko ambaye pia ni Kamishna Msaizidi wa Bajeti amesisitiza kwamba "kila mtumishi anayepewa fedha za masurufu ahakikishe mara arejeapo anafanya marejesho".

Agizo hilo lilikubaliwakwa kauli moja na wajumbe wa Kamati hiyo ambapo Mwenyekiti wake Bw. Waziri Kipacha, alitilia mkazokwa kusema " Kama Kamatitunaridhishwa na ufuatiliaji unaofanywa wa kuhakikisha masurufu yanarejeshwa kwa wakati na tunampogenza Mhasibu Mkuu kwa kulisimamia hili na kasi hii lazima iendelea".

Akijibu hoja zilizoibuliwa na Mkaguzi wa ndaniambazo ziliwasilishwa mbele ya Kamati hiyo, Bw. Kassim Chanika aliyemwakilishaMhasibu Mkuu, alisemaIdara ya Uhasibu imejitahidi sana katika kufuatilia urejeshwaji wa masurufu na kwamba zaidi ya shilingi milioni 40 masurufu yake yamerejeshwa.

Kamati hiyo pia imesisitiza kwamba, manunuzi yote ya Ofisiyanafanyika kupitiaKitengo cha Manunuzi ( PMU) badalaya kila mtu kuamua kununua kitu fulani na kuwasilisha risitikitengo cha Manunuzi.

Kamati imelisisitiza hilo ili pamojana mambo mengine kuepukamwingiliano wa majukumu, matumizi mabaya ya fedha, ukiukwaji wa sheria za manunuzi na kuleta vifaa au bidhaa ambazo hazina ubora na haziendani na thamani ya fedha.

kuhusu uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji, Kamati pia iemelekeza kwamba, kwa kila Idara na Kitengo iliyotengewa bajeti ya kutekeleza majukumu yake ni lazima itoe taarifa ya utekelezaji kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Agizo hilo limetokana na taarifa ya Mkaguzi wa Ndani kuonyesha kwamba katika Idara ambazo zimefanyiwa ukaguzi amebaini uwepo wa mapungufu makubwa yaupatikanaji wa takwimu zinazoonyesha utekelezaji wa majukumu ya idara kutokana na kutokuwapo kwa utararibu au mfumo mzuri wa kuandaa na kutunza taarifa za hizo.

Hoja yakutokuwapo kwa takwimu sahahi zinazoelezea au kuanisha kwa kina utekelezaji wa majukumu ya kila siku hasa kwa Idara za Kisheria na nyinginezo lilitolewa maelezo na baadhi ya wajumbe kwamba ni tatizo la Taasisi nzima.

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu na Ushauri wa Kisheria Dkt. Gift Kweka ambaye ni mjumbe wa Kamati hiyo, akichangia eneo hilo, alisema " ni kweli kunachangamoto za uwekaji wa takwimu na pengine si tatizo la kutokuwapo kwa mfumo balli nadhani tatizo ni mazoea".

Hata hivyo Dkt Kweka amesema, tatizo hilo limeanzakufanyiwa kazi kwa kutolea mfano wa Idara yake kujiweka utaratibu wa kila mtumishi kuwasilisha taarifa kila mwezi ya kazi alizotekeleza na atapimwa utendaji kazi wake kupitia taarifa hizo.

Naye Mkurugenzi wa Mipango,Bibi Nkuvililwa Simkanga, akichangia hoja hiyo alisema Idara yake imeanza kazi ya kuandaa mfumo wa kurekodi takwimu na kwamba mfumo huo utakapokamilika utarahisisha uaandaji na upatikanaji wa takwimu za utekelezaji wa majukumu.

kwa upande wa maoni ya jumla, Kamati ya Ukaguzi imeangiza na kushauri umuhimu wa taarifa za ukaguzi na taarifa nyingine kuwasilishwakatika vikao vya manejimenti.

Wajumbe wa Kamati hiyo walitilia mkazo kwa Menejimeni kuwa na muda wa kuzipitia taarifa hizo kwa kina na kujiridhisha na majibu ya hoja zilizoibuliwa naMkaguzi Mkuu wa Ndani kama zinakidhi na zimeandaliwa vema.

Katika hatua nyingine Kamati hiyo imempongeza Afisa Masuhuli Mkuu,Naibu Mwanasheria Mkuu waSerikali,Dkt. Evaristo Longopa kwa namna anavyotoa ushirikiano kwa Kamati hiyo kwa kuzingatia na kutekeleza maoni yanayotolewa na Kamati hiyo au na Mkaguzi wa Ndani.

Kamati imesema kuwa hoja zinazoibuliwa na Mkaguzi wa Ndani,mara nyingi zinalenga katika kuimarisha utendaji wa Taasisi na kwamba kwa Afisa Masuhuli Mkuu kusikiliza ushauri na kuzifanyia kazi hoja ni wazi kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ipo katika mwelekeo mzuri.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Ndani Mkuu, Bw. Msechu Ibrahimu ameshukurukwa ushirikiano anaoupatakutoka kwa Afisa Masuhuli Mkuu pamoja na Menejimenti nzima. Ushirikiano ambao amesema unarahisisha utekelezaji wa majukumu yake licha ya kukabiliwa na upungufu wa watumishi.

Kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kikao chakehicho, ilijadiri taarifa iliyotokana na hoja za ukaguzi,kupitia taarifa ya utekelezaji wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kwa robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Fungu la16.

Aidha Kamati pia ilipitia Mpango Kazi wa Kitengo hicho kwa mwaka 2019/2019 hoja nyingi zilizojibiwa au kutolewa ufafanuzi zilihusu masuala ya Uhasibu na Manunuzi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

5/9/2019