Habari

Imewekwa: Oct, 16 2019

MAFUNZO MAALUM KUWA ENDELEVU-AG

News Images

MAFUNZO MAAALUM KUWA ENDELEVU-AG

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Profesa Adelardus Kilangi amesema, ni matumaini yake na matarajioyake kwamba, baada ya Watumishi wa Ofisi yake kupewa MafunzoMaalum, sasa watatekelezaji majukumu yao kwa kuzingatiaSheria,Kanuni na Taratibu zaUtumishi wa Umma.

Profesa Kilangi ameyasema hayo siku ya kwanza (jumatano) ya mafunzo Maalum yaliyotolewa kwa Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Vitengo. Mafunzo hayo ambayo yanaratibiwa na Idara ya Utawala na RaslimaliWatuyanaendeshwa na Ofisi ya Usalama wa Serikali ( GSO).

Mwanasheria Mkuu wa Serikaliambaye licha ya kubanwa naratibaalifika katika Ukumbi wa Mikutano Mtumba ambapo mafunzohayo Maalum yalikuwa yakiendelea naakatumia fursa hiyo kuishukuru Ofisi ya GSO kwa kutenga muda wa kuja kutoa mafunzo Maalumukwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Ninataarifa juu ya kuanza kwa mafunzo haya,nimefika leo na ninapashwa kuhudhuria mkutano fulani, lakini nikaonavemanije niwaone na kuwashukuru kwanza, Ofisi ya GSO kwa kutukubalia ombi letu na kuja kutoa mafunzohaya ninawashukuru sana. Lakini pia niwashukurunyie wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi na wakuu wa vitengokwa kushiriki Mafunzo hayo". Akasema AG.

Akaongeza kwa kusema "Mafunzo haya yalikuwa yafanyike tangu mwaka jana lakini kwa sababu mbalimbali hayakufanyika, lakini pia nieleza kwamba mafunzo haya yatakuwa endelevu na nimatumaini yangu kwamba baada ya mafunzo haya utendaji wetu na utekelezaji wa majukumu yetu utabadilika kwa kiasi kikubwa".

Akasisitiza kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Ofisi nyeti na kwa sababu hiyo watumishi wake wanapashwa kuwajibika ipasavyo.

Profesa Kilangi pia alitumia fursa hiyo kuwasilisha salamu za Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa ambaye hakuweza kuhudhuria mfunzo hayo kutoka na kubanwa na majukumu .

Awalimkufunzi wa Mafunzo hayo Maalum, Naibu MkurugenziMkuu wa Ofisi yaUsalama wa SerikaliBi. Riziki Mtimbo pamoja na mambo mengine amewaasa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalikuhakikisha kwamba kwa namna yoyote ile wanapotekeleza majukumu yao hawatoisiri za Serikali.

Akasema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inategemewa sana na ni moja ya Taasisi nyeti kwa hiyo kila mtumishi alinde kazi yake,nyaraka, vitendea kazi na kusisitiza kwamba Kazi zinazofanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilindwekwa maslahi yaNchi na watu wake.

Akasisitiza kwamba kila mtumishi atimize wajibu wake kwa kutangulizauzalendo lakini pia kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

Mafunzo hayo yaliambatana na ujazazi wa fomu mbalimbalipamoja na kula kiapo.

Kesho tarehe 17/10/2019 mafunzo hayo yataingia siku ya pilina washiriki watakuwa ni Mawakili wa Serikali Wote, Maafisa kutoka Utawala,CA, DP, CIA, PMU na ICT.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano.