Habari

Imewekwa: Oct, 05 2021

Makabidhiano ya Ofisi

News Images

MAKABIDHIANO YAOFISI

Na Mwandishiwetu

Dodoma

AliyekuwaMwanasheria Mkuu wa Serikali, Balozi Mteule, Profesa Adelardus Kilangi,amemkabidhi rasmi Ofisi,Mwanasheria Mkuu wa SerikaliDkt. Eliezer Feleshi katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikaliiliyopo mji wa Serikali , Mtumba, Jijini Dodoma.

Katika makabidhiano hayo, Profesa Kilangi ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuuwa Serikali wa Tisa (9),amemhakikisha ushirikiano wa Karibu Dkt. Feleshikatika utekelezaji wa majukumu yake.

“Ninaomba nikukabidhi rasmi Ofisi, na nichukue fursa hiikukupongeza sana kwa kuaminiwa na Mhe. Rais kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Kumi ( 10) mpaka sasa. Nikutakie kila kheri katikautekelezajiwa majukumu yako . Mimi nipotayari kwa jambo lolote ambalo utaonapengineunahitaji institution memory basi mimi nipo” amebainishaBalozi Mteule Profesa Kilangi.

Kwa upande wake, MwanasheriaMkuu wa Serikali,Dkt. Eliezer Feleshi amemshukuruProfesaKilangi kwa makabidhianohayo, pongezi na ahadi ya ushirikiano aliyoitoa.