MAKABIDHIANO YA TUZO YA KUWA TAASISI YA PILI USIMAMIZI WA UTAWALA NA RASLIMALI WATU

Imewekwa: 17 Oct, 2023
MAKABIDHIANO YA TUZO YA KUWA TAASISI YA PILI   USIMAMIZI  WA UTAWALA NA  RASLIMALI  WATU

Na Mwandishi Maalum

Itakumbukwa katika Mkutano wa Kazi wa Wakuu wa Idara za Utawala na  Raslimali   Watu uliofanyika Mkoani Arusha hivi Karibuni. Pamoja na mambo mengine, Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu wa  Serikali  kama Taasisi inayojitegemea ilishinda Tuzo kwa  kuwa mshindi wa pili wa Taasisi  bora  inayojitegemea inayofanya  vizuri katika kusimamia utawala na  raslimali watu

Leo  Jumanne  Octoba 17/2023 Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe. Jaji Dkt. Eliezer  Mbuki  Feleshi amekabidhiwa rasmi Tuzo hiyo katika hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mtumba  Jijini Dodoma

Kabla ya MMS kukabidhiwa Tunzo hiyo,  Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Bw. Silas  Marwa  alimkabidhi  Tuzo hiyo Kaimu Naibu  Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Bw. Onorius Njole ( Kama  Mkuu wa Utawala na Raslimali  watu) na kisha naye  Kumkabidhi Mkuu wa Taasisi Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akizungumza  baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Feleshi Pamoja na kuipongeza Idara ya  Utawala na Raslimali  watu na watumishi wote wa OMMS, amesema  Tuzo hiyo  ni heshima kubwa kwa OMMS na  kutaka kazi njema inayofanywa na Taasisi kuendelea kudumishwa ili kupata Tuzo  nyingi Zaidi

17/10/2023