MAWAKILI WA SERIKALI NA WAKUJITEGEMEA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI

Imewekwa: 31 May, 2023
MAWAKILI WA SERIKALI NA WAKUJITEGEMEA WAJENGEWA UWEZO  KUHUSU MAHAKAMA YA  AFRIKA MASHARIKI

WAJENGEWA UELEWA KUHUSU YA UTENDAJI KAZI WA EACJ

Na  Mwandishi  wetu

Mawakili  wa Serikali  sita (6) kutoka Taasisi za Kisheria za Serikali  wamepata fursa ya  kuhudhuria mafunzo ya  siku mbili  ya kuwajengea uwezo na uelewa  kuhusu  majukumu ya Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).

Mafunzo  hayo  yamefanyika hivi  karibu katika Hoteli  Serena Mkoani  Dar es Salaam  ambako pamoja na  Mawakili hao wa Serikali  pia yalihudhuriwa na  Mawakili  15 wa Kujitegemea.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Mafunzo hayo Dkt. Dafina Ndumbaro  kutoka Divisheni ya Uratibu na   Ushauri wa  Kisheria ( DCAS) Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa  Serikali,  anasema katika siku hizo  washiriki wa walipata  nafasi  ya kujifunza masuala mbalimbli  yanayohusiana  na mahakama hiyo.

Baadhi ya  masuala  hayo   ni  Mkao (Set up) ya Mahakama,Mamlaka (Jurisdiction) ya EACJ,Nani anaweza kusimamia kesi katika mahakama hiyo na Muda sahihi wa kufungua shauri,

Dkt. Ndumbaro anaeleza kuwa,  washiriki hao  pia  walielimishwa  kuhusu             Mamlaka ya Mahakama za nchi Mwanachama katika mashauri yanayohusu Jumuiya ya Afrika Mashariki na  Utaratibu wa Kukata rufaa.

Vile vile  Mawakili   Serikali pamoja na  wenzao wa kujitegemea pia walijengewa uwezo   kuhusu Kanuni zinazotumika Katika Mahakama za nchi Mwanachama wanapotaka kuwasilisha kesi kwa ajili ya maamuzi katika Mahakama ya Afrika Mashariki (kwa mujibu wa Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mahariki).

“Mafunzo haya ingawa yalikuwa ya siku mbili lakini  yalikuwa na umuhimu  wa pekee kwetu kama  mawakili  wa serikali , ni mafunzo ambayo yametupa fursa ya kujifunza mambo mapya yatakayotusaidia  katika utendaji kazi wetu wa kila  siku”. Amesema  Dkt. Ndumbaro

Mawakili  wa Serikali sita   waliohudhuria Mafunzo hayo  ni Beno Sanga (PSA), Felister Lelo (SSA) kutoka OAG, Hannelore M. Mnyanga (PSA),   na Jackline Kinyasi(SA) kutoka NPS,Victoria Lugendo (SA) na Francis Oswald (SA) kutoka OSG

Aidha  Mawakili  hao wa Serikali    na Mawakili wa kujitegemea wameishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa  kuratibu  mafunzo hayo kwa kushirikiana na Mahakama ya Afrika Mashariki.

Imeandaliwa na  Kitengo cha Mawasiliano

31/5/2022