Habari

Imewekwa: Jan, 29 2020

Mazugumzo ya kujengeana uwezo

News Images

MAZUGUMZO YA KUJENGEANA UWEZO

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt.Evaristo Longopa,(DAG) amekutana na kufanya mazungumzo na wataalamu kutoka RTI International.

Mazungumzo kati DAG na wataalamhao, Bw. Dawie Pieterse na Bi. Lauren Divenanzo, yamefanyika leo (Jumatano)katika OfisiyaMtumba,na yalihusu namna ya pande hizi mbili zitakavyoweza kushirikiana katika mafunzo ya kujengeana uwezo katika Sekta ya Nishati.

“Tumekuwa na majadiliano mazuri, kimsingi walikuja ili tubadilishanemawazo ya namna na maeneno ambayotunaweza kuwajengea uwezo wanasheria wetu katika Sektaya Nishati”. Anabainisha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali mara baada ya mazungumzo hayo.

Kwa mujibu wa Dkt. Longopa, wataalamu haokutokaRTI International ni watekelezaji wa programu za kusaidiaSekta ya Nishati kwa Nchi za Afrika Mashariki ijulikanayo kama East Africa Energy Program (EAEP) na wapo nchini kuboreshamaeneo yakuisaidiaTanzania katika Sekta ya Nishati kwa miaka miwili ijayo yakiwamo maeneo ya kujengeana uwezo.

Programu hii ya EAEP inasimamiwa na Shirika la MaendeleolaMarekani (USAID). Aidha kupitia programu hii USAID imekuwa ikilisaidia Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na wadau wengine wa Serikali katika maeneo yaMikataba ya Nishati na Mikataba ya Manunuzi (Power Purchase Agreements)

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia naMkurugenzi wa Uratibu na Huduma za KisheriaDkt. Gift Kweka na Bw. John Kabi kutoka USAID

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano