Habari

Imewekwa: Sep, 04 2019

MSISUBIRI KUSUKUMWA -DAG

News Images

TEKELEZENI MAJUKUMU YENU MSISUBIRI KUSUKUMWA-DAG

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG), Dkt Evaristo Longopa, amesema haipendezi kwa Mkuu wa Idara au Kitengo kusukumwa ndipo atekeleza majukumu yake.

Ametoa kauli hiyo leo (jumanne) wakati akifungua kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma.

Katika kikao hicho ambachokilianza kwa uwasilishwaji wa Taarifa yaRobo Mwaka ya utekelezaji wa Mpango wa Manunuzi, na kufuatiwa na kikaokilichojadili Mgao wa Matumizi ya Fedha kwa Mwezi Agost, 2019. Naibu Mwanasheria Mkuu amesisitiza sana umuhimu wa kila Mkuu wa Idara na Kitengo kuwajibika.

“ Nimekuwa nje ya ofisi kwa miezi miwili na hiki ni kikao changu cha kwanza cha menejimenti, nianze kwa kusema, katika mwaka huu wa fedha ( 2019/2020) kila mtu atimize wajibu wake ipasavyo. Tusiende kwa kusukumwa haipendezi” amesisitiza Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Na kuongeza “tushirikiane kwa kuhakikisha kwamba, kama ulitakiwa kufanya jukumu fulani katika Idara yako au Kitengo chako basi fanya hilojukumu usisubiri mpaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Naibu Mwanasheria Mkuu akusukume kutekeleza hayo majukumu yako”.

DAGameileza menejimenti hiyo kwamba,anaamini kuwa kila moja akitekeleza majukumu yake kwa kadiri ya uwezo wake na kukiwa na ushirikianomiongoni mwao basi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Taasisi itafika mbali.

Wakati huo huo Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewashukuru watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanavyoendelea kushirikianakatika mambo mbalimbali.

Dkt Longopa amesema, ushirikiano wa hali na mali ambao watumishi wameuonyesha wakati Mkuu wa Taasisi, Mwanasheria Mkuu wa SerikaliProfesa Adelardus alipofiwa na Mke wake umempa faraja kubwa sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Ushirikiano mlioonyesha umempa faraha kubwa sana AG, ninaomba ushirikiano huu uedelee, nitumie pia fursa hii kuwashukuruwatumishi wa Idara ya Uandishi wa Sheria kwa kutoa watumishi wawili wakiungana na mtumishi mwingine wa Moshi kumsindikia mtumishi mwenzao Aptat Mrina ambaye amefiwa na Baba yake Mzazi”.

Akasema, ushirikiano aina hii ni muhimu sana kwa maana tunaishi kama familiana matatizo na chanagamoto haziwezi kukosekana hivyo basikama wafamilia tunawajibu wa kushirikiana kwa hali na mali.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

3/9/2019