Habari

Imewekwa: May, 03 2019

Mwanasheria Mkuu wa Serikali akutana na Uongozi wa TLS

News Images

SERIKALI KUSHIRIKIANA NATLS-

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi,amesema, Serikali inatambua mchango wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika ( TLS) katikakuimarisha na kudumisha Utawala wa Sherianchini.

Akasemawakati woteSerikali ipo tayari kupokea maoni na ushauri kutoka TLS ilimradi kwamba,maoniau ushauri huo unajikita katikakujenga, kuimarisha, hauegemei upande wowote, wenye staha nausio na mashinikizo.

“ Kwanza niwashukuru sana kwa kuja kukutanana kufanyamazungumzo nami, niwapongeze wewe Rais kwa kuchaguliwakuwa Rais wa TLS pamojanawotemliochaguliwa katika baraza la uongozi.Ni matumaini yangu kwamba, hamtawaangushawanachama wenu waliowachagua, msiwaagushe tafadhali”AkasemaMwanasheria Mkuu wa Serikalinakuongeza

“Wakati wote Serikaliimekuwa ikithamini sana mchango wenu na maoni yenu. Na kwa kweli mmekuwa mkitoa mchangona maoni mazuri sana, niwahakikishe kwamba Serikaliwakati wote ipotayari kushirikiana nanyi. Jambo la muhimu nikuwa namajadiliano ( dialogue) pale ambapomnaonakunajambo la kujadiliana kabla yakulitolea matamko.

“Niwahakikishe kwamba, Serikali kwa ujumla na hasa Mhe. Rais John Pombe Magufulikatikauongozi wake anapenda sana Sheria na anatakamambo yafanyike kisheria na kwa kuzingatia sheria ” akasisitiza Profesa Kilangi

Profesa Kilangi ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumza naujumbe waBalaza la Uongozi la TLSlikiongozwa na Rais wake Dk. Rugemeleza Nshala.

Mazungumzokati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali naUjumbe wa Balaza laUongozi yaliyochukua zaidi yamasaa matatu, yalifanyika siku ya Alhamisi katikaukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mitumba- IhumwaJijini Dodoma.

“Niwaombe sana katika uongozi wenu msimamie sanawelediwa tasnia ya Sheria, hili nawaomba sana, sisi sote nimaofisa wa Mahakama, ni katika mkutadha huu tunatakiwa kutekelezamajukumu yetu yauofisa Mahakama kwa welidi wa hali ya juu sana na kwa kuzingiatia misingina maadili ya kazi zetu. Lisimamieni sana hili, simamie professionalism” akasisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais wa TLS Dk, Rugemeleza Nshalapamoja na kumshukuru Mwanasheria Mkuu waSerikali kwa kuwakubalia ombi laona kukutana nao. Alisema kunamambo kadhaa ambayo walitamani au waliona ni vema wakabilishana naye mawazo.

Dk Nshala aliyataja baadhi yamambo hayo kuwa nipamoja na kuangalia namna bora itakayowawezesha TLS nawadau wengine waSheria nchini, akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali yakushirikianakatika kuhakikisha kwambaMawakili wa kujitegemea na Mawakili wa Serikali wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa kuzingatia maadili na miiko yakazi zao.

Jambo jingine ambalo Dk. Nshalakwa niaba ya jumbe wake aliliwasilisha kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikalinila namna ya kuangaliajinsi ya kuifanyia marekebisho baadhi yavifungu vya SheriayaTLS hasa katika kifungu cha uchaguzi wa Viongoziunaotakiwakufanyika kila mwaka.

“Katikamkutano wetu wa Arusha wanachama tulilijadili hili la uchaguzi wa kila mwaka, ni hitajio la kisheria lakini gharama za kukutana kila mwaka ni kubwa sanana zinabebwa na wanachama, hivyo tulijadiliana kuonanamna gani tunaweza kuliboresha hili kwa kujadiliana na wadau wengine na kwa kuangalia mifano ya nchi nyingne akasema “ Rais wa TLS.

Dk. Nshala pia alizungumzia kuhusu mitaala yamafunzoSheria katikaVyuo Vikuu na kushauri kwambawadau wa Sheria wanapashwa kukaa na kujadiliana namna bora yakuuboresha ili iendane na wakati.

Kwa mujibu waRais huyo wa TLSamesema kwa uzoefu wake na katikautekelezaji wa majukumuyake kuna mifano haiya mapungufu ya kiutendajikwa kwa baadhiya mawakiliambayo mengikatiya hayoniukosefu wa mafunzo Stahiki

Katika hilolauboreshaji wa mfumo wa ufundishaji, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema anakubaliana nalo kwa asilimia kubwa, na kwamba , tatizo ambaloyeye analiona ndiyo changamoto kubwa katika tasnia ya Sheria ni mafunzokwa vitendo.

Mwanasheria Mkuu waSerikali Profesa Kilangi naUongozi wa TLS walijadili pia kuhusu namna bora yakuhakikisha kwambaSheria zinazofanyiwa urekebu namara zikisha pitishwa naBunge Ofisi ya Mwanasheria Mkuu isisambazeili zinawafikia wadaukwa wakati.

Vile vile walibadilishanamawazo kuhusuhaja na umuhimu wakuzifanyia urekebubaadhi ya Sheria ambazo zinamatatizoau changamoto katika utekelezaji wake.Baadhiya Sheria hizo nipamoja na baadhi ya vifungu vya Sheria ya Jinai naSheria ya Usuluhishi wa migogoro nje ya Mahakama.

Walibadilishana mawazo pia kuhusu mazingira ya utendajikazi wa Mawakili hasa mawakili wa kujitegemea ambaoDk. Nshala alisemawanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazopashwa kutafutiwa ufumbuzi.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa naNaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa naMkurugenzi wa Idara yaUratibu naUtoaji wa Huduma Dk. Gift Kweka.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Dodoma

3/5/2019