Habari

Imewekwa: Nov, 03 2021

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Feleshi akila kiapo cha uaminifu Bungeni

News Images

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Feleshi jana ( Jumanne) alikula kiapo cha uaminifu Bungeni, mwanzoni mwa Kikao cha Kwanza na Mkutano wa Tano wa Bunge Jijini Dodoma,

AG Feleshi aliapishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai pamoja na wabunge wengine wawili Emmanuel Cherehani kutoka Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga na Mohammed Said Issa wa Jimbo la Konde.