Habari

Imewekwa: Nov, 25 2019

NMB WAIPATIA OFISI YA AG COMPUTA 3O

News Images

NMB WAIPATIA OFISI YA AG COMPUTA 3O

NaMwandishi Maalum,

MwanasheriaMkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi,(AG) amesema,Komputa 30 ambazo zimetolewana Bank ya NMBzitasaidia sana katika kuimarisha nakuboreshautendaji kazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja naOfisi zake za Mikoani.

AG Kilangiameyasema hayo leo, wakati wa hafla fupiya makabidhiano ya Komputa hizo iliyofanyika katika Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoani Dar es Salaam, tukiolililoshuhudiwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa na Watumishi waOfisi hiyo Mkoani humo.

“ Kwa niaba yangu na Ofisi yoteya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,nipende kuishukuru sana NMB kwa ufadhilihuu wa vitenda kazi ambao utaimarishanakuboresha utekelezaji wa majukumu yetu” . Akasema AG

Na kusisitiza. “Kwa kuwaOfisi ya AG ina matawi katika mikoa yote, basi kwa ufadhili huu bilashaka sasa kilaMkoa utakuwa na Komputa yake na hivyo kuogeza tija kwa Mawakili wa Serikaliwaliopo katika Mikoa hiyo.

AkikabidhiKomputa hizokwaniabaya NMB, Katibu wa NMB, Lilian Komwihangiro amesema,NMB wanatambua kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalini mdau mkubwa wa Banki hiyo na kwa sababu hiyo, wanajisikiana wanawiwa kusaidia katikajuhudi za kuboresha utekelezaji wa majukumu yake.

Vile vile Komwihangiro ambaye alifuatana na Bw. Aloyce Baba ( CSR Manager) na Bw. Prosper Mwanyamila ( Mwanasheria), ameelezea utayari wa Timu yao ya Tehama kushirikiana na wataalam wa Tehama wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katikauendeshaji waKomputa hizo.

Upatikanaji wa vitendea kazi vya kutosha na vya kisasa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni moja ya hatua ambazo Mkuu wa Taasisi hii Profesa Kilangi kwa kushirikiana naNaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amekuwaakilitilia mkazo kwa kuchukua hatua mbalimbali.

25 Nov 2019