Habari

Imewekwa: Nov, 24 2021

OFISI YA MWANASHERIA MKUU NI NYETI NA YENYE DHAMANA KUBWA KWA SERIKALI- PINDA

News Images

OFISIYA MWANASHERIA MKUU NI NYETI NA YENYE DHAMANA KUBWA KWA SERIKALI- PINDA

NaMwandishi Maalum

Mwanza

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geophrey Mizengo Pindaamewataka Watumishi wa OfisiyaMwanasheria Mkuu wa Serikali, kutambua uzito na dhamana ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika uendeshaji waSerikali.

Ameyasema hayo leo ( Jumanne) Wakati alipokuwa akifungua Mkutano wa siku mbili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Baraza hilo linafanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jengola TMDAMkoani Mwanza.

Akasema, kwa mujibu waMajukumuambayo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepewa Kikatiba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuuninguzo namhimili wa uendeshaji wa Serikali na kwamba ufanisi wa serikali kwenye masuala yakisheria unawategemea sana watumishi wa Ofisi hiyo.

“Kwa muktadha huu, nivema mtambue kuwa mmpewa majukumu nyeti, na mmebeba dhamana kubwa ya kuiwezesha Serikalikutekeleza majukumu yake, na nyinyi ndiyo taswira ya Taifa letu kwenye masuala ya Utawala na Sheria” amesisitiza Naibu Waziri Pinda.

Aidhaametoa rai kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha kwamba wanaendelea kutekeleza majukumuyaokwa weledi na uadilifu wa kiwango cha juu na kwa maslahi mapana ya nchi.

“Kwa kufanya hivyo mtaiwezesha Serikali kupata ushindi kwenye kesi nyingi na kupunguza migogoro ya kisheria baina ya Serikali na Wabia” amebainisha Naibu Waziri.

KatikaBaraza hili la Wafanyakazi ambalo Mwenyekiti wake niMwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Eliezer Feleshi, NaibuWaziriPinda pia ameitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuendeleza juhudi za Serikali za kuondokana naSheria zenye mianya ya rushwa kwa kuandaa Mikataba yenye tija na inayozingatia maslahi ya Taifa.

Vile vile Naibu Waziri Pinda amesisitiza watumishi wa Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali kuvitambua vipaumbele vya Serikali ya awamu ya Sita na jinsi gani vipaumbele hivyo vinatekelezwa kwa kuzingatia majukumu yaOfisi.

Pamoja nakusisitiza matumizi yalugha ya Kiswahili katika utoaji haki, pia amesisitiza umuhimu kwa watumishi kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo ya kiutumishi na kiutendaji, ikiwa ni pamoja nakuweka mfumo wa kufutailia utendaji wa wanasheria wote wa Serikalina mpango wa Mawakili wote kupata uzoefu wa kazi mahakamani.

AwaliakimkaribishaNaibu Waziri wa Katiba na Sheriakufungua mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Eliezer Feleshi, amesema, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalihaitamvumilia mtumishi yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa.

“ katika eneo hili la uadilifu, niwasihi watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Muu wa Serikali mnatakiwa kutekeleza majukumu yenu ya kazi kwa kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma,Sheria na Kanuni. Mla rushwahata vumiliwa hata kidogo” akaonya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kuhusu idadi ya watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Feleshi amesemakwa mujibu wa Muundo wa Ofisi, Ofisi inahitaji kuwa na watumishi 477 ili kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika mikoa yote 26.

“Mhe Naibu Waziriwatumishi waliopo sasa ni121,kati hao Mawakili wa Serikali ni 54na watumishi wa kada nyingine ni 67, idadi hii ya watumishi hasa Mawakili wa serikali ni ndogo sana ikilinganishwa na mahitaji ya mawakili wa Serikali 241 wanaohitajika kutokana na kuongezeka kwa majukumu ya Ofisi katika maeneo ya upekuzi wa mikataba, Uratibu wa Huduma za Ushauri wa Kisheria na Uandishi wa Sheria.

Dkt, Feleshi amesemaOfisi imeendelea kuchukua hatua mbalimbali zakuongeza watumishi kwa kutenga nafasi za uhamisho na ajira mpya kwenye Ikama kila mwaka na kuwasilisha Ofisi ya Rais,Utumishina Utawala Bora kwa Hatua zaidi.

Amebainisha kwamba sualala uhaba wa watumishi haupo tu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali bali pia ni tatizo ambalo pia linazikabili Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na kwamba zoezi la kukamilisha uchambuzi wa mahitaji ya watumishi kufuatia mahitaji halisi ya huduma za kisheria zintolewazo na ofisi hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheriaili kwenda na mgawanyo wa maeneo ya kiutawalaSerikalini.

Mkutano wa Baraza laWafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali unahudhuriwa naWanachama 45 wa TUGHE pamoja nawajumbe waalikwa wakiwamomawakili wa Serikaliwanaosimamia Ofisiza Tabora, Dar es Salaam,Tanga,Mwanza,Arusha, Kilimanjaro ,Mbeya, Mtwara na Kagera.