OMMS YASAINI MAKUBALIANO NA TAASISI YA LAWS.AFRICA

DODOMA-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo ( alhamisi) imesaini Makubaliano ( MOU) baina yake na Taasisi ya LAWS.AFRICA.
Hafla ya utiaji Saini wa makubaliano hayo imefanyika katika siku ya kwanza ya Warsha ya siku mbili kuhusu utoaji na upatikanaji endelevu wa sheria kwa njia ya Kijiditali. Warsha hiyo imefunguliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro
Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi mara baada ya kusaini makubalino hayo kwa niaba ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalia, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa amesema, Makubaliano hayo yanahusu ushirikiano kwenye masuala ya kuwezesha Sheria zinatotungwa na Bunge na sheria ndogo kupatikana kwa urahisi kwa njia za kijiditali.
Dkt. Longopa amebainisha kwamba makubaliano hayo yataongeza na kuboresha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hasa katika kuhakikisha kwamba sheria ambazo zimefanyiwa urekebu na zile ambazo zimefanywa tafsiri kwa lugha ya kiswali zinawafikia wananchi kwa urahisi na wakati wowote.
“makubaliano haya yatutasaidia sana siyo tu kuhakikisha kwamba sheria zinapatikana kwa urahisi kwa njia ya kidijitali lakini pia zinapatikana zikiwa na marekebisho yote yaliyofanyika” akasema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Na kuongeza kuwa makubaliano hayo yatahusu pia kubadilishana uzoefu na uwezeshaji kwa njia ya mafunzo katika Chuo Kikuu cha CAPE- TOWN.
Aidha Pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kusaini makubaliano nayo vilevile Tume ya Kurekebisha Sheri nayo imesaini Makubaliano hayo.
Warsha hiyo ya siku mbili imeandaliwa na GIZ, African Lii na LAWS . AFRICA na washiriki wake ni Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Seriali, Tume ya Kurekebisha Sheria, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika ( TLS) Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Seriali na Wizara ya Katiba na Sheria.
Ajenda au mada kuu ya Warsha hii ni utoaji endelevu wa sheria za Tanzania kupitia mifumo ya Kidijitali.