Habari

Imewekwa: Dec, 03 2021

SUMAJKT ALIPWA Bilioni 4. UJENZI WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

News Images

SUMAJKTALIPWA Bilioni 4. UJENZI WA OFISI YAMWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Na Mwandishi Maalum

Dodoma

Mkandarasianayejenga awamu ya piliyajengo laMakao Makuu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa SerikaliDodoma, hadi sasa amekwishakulipwa na Serikali shilingi Bilioni nne na elfu ishirini na mbili (4,022,000,000) kama malipoya awali

Kwa mujibuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Eliezer Feleshi ambaye alitoa taarifa za kufanyika kwa malipo hayo, amesemaujenziwaJengohilo upo katika hatua za uchimbaji wa msingi na kwamba tayari serikali ilikuwa imekwisha kutoa kiasi hicho cha fedha.

Jana (Alhamisi) Mwanasheria Mkuu wa Serikalialikuwa miongoni mwa Viongoziwaliohudhuria hafla yauzinduzirasmi wa ujenzi wa awamu ya pili ya Majengo 24 ya Wizara na Taasisi mbalimbaliunaoendeleakatika Mjini wa Serikali – Mtumba.

Hafla ya uzinduzi wa ujenzihuo na ambayo pia iliambatana na uzinduzi wamaadhimisho ya miaka 60 yaUhuru waTanzania bara kitaifa, ulifanywa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

Kwa mujibu Waziri Mkuu majengo hayo 24 yenye ghorofa kuanzia3 na kuendelea, serikaliimeidhinisha kiasi cha Sh. Bilioni 300, kwajili ya ujenzi huo

Jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalikwa mujibu yamichoro iliyopitishwa, litakuwa na umbo lenye kufanana na herufi Y, likiwanaghorofa tano nalinajengwa naKampuni ya Uhandisi na Ujenzi ya SUMAJKT.

Mpaka kukamilika kwakejengo hilolitagharimu shilingi Bilioni 26.8

Kwa umbo lake, Jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalilitakuwakati yaJengo litakalokuwana muonekano tofauti na majengo mengine ya Wizara na Taasisiyanayoendelea kujengwa katika Mji wa Serikali - Mtumba

Katika eneo la Ujenzi waOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalishughuli mbalimbali zinaendelea nabaadhi ya vibarua ambao wamepata ajirani pamoja na wanawake ambao baadhi yao wameonekanawakiwa wamebeba ndoo za maj pamoja nakufanya shughuli nyinginezo.