Habari

Imewekwa: Sep, 09 2021

SUMAJKT KUJENGA JENGO LA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

News Images

SUMAJKT KUJENGAJENGO LA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI-MTUMBA

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, amemtaka Mkandarasi ambaye amekabidhiwakandarasi ya ujenzi wa awamu ya pili Jengo jipyala Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo kwa wakati , kwa viwango na uboraunaokubalika.

Ameyasema hayo wakati wa haflafupi ya utiaji saini mkataba wa ujenzibaina yaOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT. Hafla hiyo ilifanyika jana ( Jumatano) Jijini Dodoma.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopandiyo aliyesainimkataba huo kwa upande wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa upande wa Mkandarasi ( SUMAJKT)ulisainiwa na Meja Samweli S. Jambo ambaye ni Mkurugenzi wa Uhandisi na Ujenzi wa Kampuni hiyo.

Profesa Kilangi, alizipongeza pande zote mbili kwa kusainina kukabidhiana mkataba wa ujenzihatua mbayo amesema sasa inaashiriakuanza kwa kazimapema iwezekanavyo.

“Leotulikuwa na Kikaona Waziri Mkuu kuhusiana na suala hili la ujenzi wa awamu ya pili ya Majengo ya Serikali katika Mji wa Serikali wa Mtumba, na moja ya maagizo aliyotoa nikuanza kwa ujenzi wa majengo yote ifikapomwisho wa mwezi huu wa Septemba. Sisi leotumesaini mkataba wa ujenzi ni matumaini yangu ndani yawiki hii au ijayonitaona vumbi likitimka katika eneo la Ujenzi” amesemaMwanasheria Mkuu wa Serikali

Na kuongeza kwamba, Ofisiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imeamua kuichagua na kuipitisha Kampuni ya Ujenziya SUMAJKT, kutokana narekodi yake yautendaji katika maeneo mengi, kukamilisha kazi kwa wakati na wakati mwingine hata kabla ya wakati.

“Hatukufanyakwabahati mbaya kuwachagua, ni rekodi yenu na niwapongeze kwa kuteuliwa kwenu, lakini pamoja na pongezi hi, ni matumini yangu kwamba, mtatoa kipaumbele namsukumowa kipekee iliujenzi wa Jengo letu uende kwa wakati, kwa viwango vinavyotakiwakwa kuwa mnao utaalamu,mnanyezo , mna watu na nidhamuya hali ya juu,”.

AidhaProfesa Kilangi,amesisitizaumuhimu wa Kampuni hiyo kuhakikisha wanazingatiaviwango na ubora wavifaa vya ujenzi watakavyotumia.

AkaitakaMenejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuhakikisha kwamba, inatimiza wajibu wake iliisiwe kikwazo kwa Kampunihiyo ya Ujenzi na hivyo kuchelewesha au kukwamisha kazi.

Akabainisha kwambakwa mujibuwa WaziriMkuu, Mhe. Rais ameshatoa idhini ya fedha zaujenziwa awamu ya pili , ujenzi ambao amesemautabadirishasura ya Mjini wa Serikali Mtumba naJiji la Dodoma.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenziya SUMAJKT, Meja Samuel Jambo,pamoja na kushukuru kwa Kampuni yake kupewa kazi ya ujenzi huo, amemuhakikishaMwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba,watajitahidi kuifanya kazi hiyo kwa weledi, viwango na ubora unaotakiwa na ikiwezekana kuikamilishakazi hiyo hata kabla ya wakati.

NayeNaibuMwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Longopa, amesema,Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikaliitatoa ushirikianokwa mkadarasi ilikuhakikishahakuna kunachokwama katika utekelezaji wa mradi huo.

Utiaji saini wa Mkataba huo,mbali na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ulishuhudiwapia naMwandishi Mkuu wa Sheria,Bw. Onorius Njole, Mkurugenzi wa Utawala na RaslimaliWatu Bw. Jackson Nyamwihula naBw. Vedastus Shibugulu Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugav.

Ujenzi waawamu ya Pili yaJengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lenye ghorofa tano, na litakalojengwa katikaumbo ya herufi Yutaghalimukiasi cha shilingiBilioni26.8. litakapokamilijengo hili litakuwa Jengolenye muonekanotofauti na majengo mengine kutokana na umbo lake.

Pamoja nakutiwa sainikwaMkataba wa Ujenzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pia ilitiliana saini na msimamizi wa Ujenzi wa Jengo hilo ambaye niWakala wa Majengo ya Serikali( TBA)

Naibu Mwanasheria Mkuu wa SerikaliDkt. Evaristo Longopa ndiye aliyesainikwa upande wa Ofisi na kwa upandewa TBA alisaini Mtendaji Mkuu, Bw. Daud Kondoro.