Habari

Imewekwa: Jul, 24 2019

TCRA WAKABIDHI KOMPUTA 10 OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

News Images

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI APOKEA AWAMUYA KWANZA YA VIFAA KUTOKA TCRA

Na Mwandishi wetu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA) imeanza kutekeleza ahadi yake ya kuisaidiaOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali vifaa mbalimbali.

Jana (jumanne) TCRA kupitiaMwakilishi wake, Bw. Johannes Karungura ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria katika Mamlaka hiyo, alikambidhi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adeladus Kilangi vifaa mbalimbali zikwamo Komputa za mezani 10 na meza zake.

Hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo ambavyoni awamu ya kwanza, ilifanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoani Dar es Salaam, na kushuhudiwa na Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Kandaya Dar es Salaam.

Akikabidhi vifaa hivyo, Bw. Johannes Karungura, amemweleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Kilangi, kwamba, Mamlaka hiyo inafarijika sana kuwasilisha vifaa hivyo kama ilivyoahidi na kwamba itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kila itakapowezekana.

Akasema, TCRA imekuwa mnufaika mkubwa wa huduma zinatolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Huduma ambazo amesemazinatolewa kwa haraka, ufanisi na kwa wakati na kwa sababu hiyo wataendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikli ili pamoja na mambo mengine iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Akipokeavifaa hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, pamoja na kuishukuru TCRA, pia amesema vifaa hivyo vitasaidia sana kuchagiza utendajikazi na uboreshaji wa mazingira ya kazi.

“Naomba niwashukuru sana kwa msaada wenu, naomba msituchoke kwa sababu tutaendelea kuomba ushirikiano wenu.Lengo ni kuboresha mazingira ya utekeleji wa majukumu yetu kwa kuwa na vitendea kazi vya kutosha ili kupitia uboreshaji huo basi utekelezaji wa majukumu yetu uwe wenye tija zaidi na viwango vinavyokubalika” amesisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikal.

Na kuongeza kuwa, baadhi ya vifaa hivyo vitabaki katika Ofisi ya Mkoa wa Dar esSalaam na vingine vitepelekwaMakao Makuuya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jijini Dodoma.

Vifaa vingine vilivyokabidhiwa jana pamoja na computa hizo kumi na meza zake ni CCTV, colour printers na computer softaware.

Itakumbukwa kwamba, akizungumza kwa nyakati tofauti, katika vikao kazi na Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jijini Dodoma mwishoni mwa mwezi June, pamoja na masuala mengine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi, alieleza kwamba, uongozi unachukua hatua mbalimbali zinazolenga kuboresha mazingira ya utendaji kazi.

Akafafanua kwamba katika kukabiliana na uhaba wa vitenda kazi tayari alikuwa amewasilisha ombi TCRA ya kupatiwa Computa 40 pamoja na vifaa vinginevyo. Ombi alilosema TCRA walikuwa wakilifanyia kazi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

Julai 24,2019