Habari

Imewekwa: Jul, 02 2021

TUGHE TAWI LA OFISI YA MWANASHERIA MKUU YAPATA VIONGOZI

News Images

TUGHE TAWI LAOFISI YA MWANASHERIA MKUUYAPATA VIONGOZI

Na Mwandishi wetu

Naibu MwanasheriaMkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa,amewatakaViongozi waChama cha Wafanyakaziwa Serikali naAfya (TUGHE) Tawi la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuwahimiza wanachama waokujiendeleza kwa mujibu wa taaluma zao.

Ametoa wito huo leo ( Jumatano) wakati akifungua Mkutano wa Uchaguzi waViongozi wa Tawi la TUGHE, uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa MikutanowaOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa SerikaliMtumba na kusimamiwa na Katibu wa TUGHEMkoa wa Dodoma, Bw. Anthelemus Tarimo.--

Akasemakujiendeleakitaalumakwa mtumishi au mfanyakazi yoyote ni wajibu wa kwanza wa mtumishi mwenyewe. Akaenda mbali zaidi kwa kusema,wapo baadhi ya watumishi ambao pengine hawataweza kupandishwa madaraja kwa sababu ya kukosasifa moja ama mbali.

“ Mwajirihawezi kumlazimisha mtumishi akasome,anatakiwa yeye mwenyewe aone hajanaumuhimu wa kujiendeleza, jukumu letu kama Mwajiri ni kusaidia na kumwezesha aende akasome. Sasa nyinyi viongozi wa TUGHE mna wajibu wa kuwahimiza wanachama wenu wakajiendeleze ili wasikwamelinapokuja suala la kupandiwa madaraja kwa sababu tu amekosa sifa.

Akizungumziakuhusu aina ya viongozi ambao wanachama walitakiwa kuwachangua,Dkt Longopa, aliwaasa kuchagua viongozi wachapa kazi, waadilifu, wenye nguvu na uwezo wa kujenga hoja, na kutetea maslahi yawanachama wao.

“ Mkichagua viongozi goigoi na legelehawataweza kujenga hoja za kutetea maslahi yetu, kwa hiyo tumieni haki yenu ya kuchagua na kuchaguliwa vizuri.

Aidhaamewataka viongozi haokujitahidi kuongeza idadi yawanachama, na kwambautaitishwakikao maalumu katika mwaka mpya wa fedhakikao ambacho ajenda yake itakuwa ni kuhamasisha wanachama wapya.

Akaahidi kuendeleza ushirikiano, majadiliano na maelewano na Viongozi wa Tughekatikamasuala mbalimbaliyanayohusu watumishi,na utekelezaji wa majukumu ya Taasisiili kuleta tija na ufasini na akashukuru kwa ushurikianomzuri uliopo baina ya Tughe Tawi la Uongozi.

Tawi la TUGHE la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali linawachama45.

Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzihuo uliosimamiwa na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Anthelemus Tarimo ni Bw. Paschal Mkungwa ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tawi kwa kupata kura 17.

Kwa upande wa nafasi ya Katibuwa Tawialiyechaguliwa ni Bi. Dorina Kalumna aliyepata kura 10 .

Wanachama hao wa TUGHE pia walipiga kura za kuwachagua wajumbewatatu wa Halmashauri ya Tawi.Walioshinda na kura zao kwenye mabano niBi. Kalua Kanyika(13), Bw. Mohammed Kilenga (16) naBw. Seleman Mwinyimkuu(16).

Kwa upande waMwakilishi waVijana nafasi hiyo imechukuliwa na Bi. Rehema Diwanialiyekuwa mgombea pekeena hivyo kujizoleakura zote 17.

Bi.Rehema Msemo yeyealijizolea kura zote 17 za ndiyo na hivyo kuchaguliwa kuwaMwakilishi wa Wenye Ulemavu.

Katika hatua nyingineWanachama Wanawake wa TUGHE nao walifanya uchaguzi wa Mwenyekiti waKamati yaWanawake, Katibu, Mweka Hazina na Wajumbe wa Kamatiwawili .

Aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti niBi. Evalight Mlay, huku nafasi ya Katibu ikienda kwa Bi. Shamila Njovu nanafasi ya Mweka hazina ikienda kwa Bi, Jane Mlay. HukuBi.KulthumHamidu naBi. Grace Assenga walipitishwa bila kupingwa katikanafasi ya Wajumbe wa Kamati yaWanawake.

Wagombea wanafasi hizolicha yakupiga kampeni za hapa na palezikiwamo za kuwaandalia chai wajumbe,lakini pia walijiandaa vilivyokwakufanya mazoezi yanamna ya kuongea na kuomba kurakwawajumbe.

Mwanachamaanayetaka kugombea nafasi ya uongozi wa TUGHE anapashwa awe amelipa ada yaUanachama kwa muda wa miezi kumi na mbili mfululizo.