Habari

Imewekwa: Nov, 10 2020

TUMEAMINIWA TUCHAPE KAZI-AG KILANGO

News Images

TUMEAMINIWA TUCHAPE KAZI- AG KILANGI

Na Mwandishi wetu, Mtumba-Dodoma

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prpofesa Aderladus Kilangi,amesema, kuaminiwa kwake na ‘Mamlaka’ kiasi cha kuteuliwa tena kuendelea kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikalikwa kipindi cha miaka mitano mingine, ni dhamana kubwa kwake na kwa Ofisi nzima ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Na kwa sababu hiyo,Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amewaasa watumishi wote wa Ofisi yake kuendelea kufanya kazi kwa juhudi kubwazaidi, kujitumana kwa maarifa zaidi.

“Nimeaminiwa, na mimi ninawaamini sana, tumeaminiwa, tuna kazi kubwa sana mbele yetu, kuna kazi ambazo bado hatujazimaliza tunatakiwa tuzimalize, lakini pia kuaminiwa huku kunatufanya tupewa kazi au majukumu mengi sana ambayo mengine si ya kwetu. Ninawapongeza sana na ninawashukuru sana nawaomba tuchape kazi” akasema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ameyasema hayo jana (jumatatu) wakati alipozungumza na wafanyakazi wa Ofisi yake waliojipanga nje ya Ofisi(Mtumba) kumlaki na kumpongeza muda mfupi tu baada ya kuwa ameapishwana Mhe. Rais John Pombe Magufuli.

Kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ambaye anakuwa mteule wa kwanza tangu Mhe. Rais na Makamu wake walipoapishwawiki iliyopita, sasa kunaashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Serikali.

Katika mapokezi hayo, Wafanyakazi hao wakiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa,wakiwa wamejaa bashasha waliimba wimbo kwa kuwa na Imani na Kiogozi wao, na kisha kumkabishimaua na kadi ya pongezi iliyokuwa imesainiwa na watumishi hao kila mmoja akiandika ujumbe wa kumtakia kila lililojema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pamoja nakuzungumza na watumishi katika ujumla wao, Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia alikata keki maalum aliyokuwa ameandaliwana kisha kuendesha kikao kufupi cha Menejimenti.

Wakati huo huo leo Jumanne, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zoezi la kuapishwa kwa wabunge wapya, lilianza baada ya kukamilika kwa zoezi la kupiga kura ya kumchagua Spika. Katika zoezi hilo Mhe. Job Ndugai alipigiwa kura zilizomwezesha kuwa tena Spika wa Bunge kwa miakamingine mitano.