Habari

Imewekwa: Dec, 17 2019

UONGOZI NI KUPOKEZANA KIJITI-DAG

News Images

UONGOZI NI KUPOKEZANA KIJITI -DAG

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Dkt.Evaristo Longopa, amesisitiza haja na umuhimu kwa Watumishi wa Idara ya Mikataba (DCT) na Watumishi wote katika Ofisi yaMwanasheria Mkuu waSerikali, kudumisha ushirikiano na uhusiano ili Ofisiiweze kufikia malengo yake.

Ametoa msisitizo huo leo ( Jumatatu) wakati wa makabidhiano ya Ofisiya DCT baina ya Kaimu Mkurugenzi Bi.Ndeonike Mwaikambo na Mkurugenzi mpya Bw. Francis Kayichile ambaye ameteuliwa hivi karibu kushika nafasi hiyo.

Dkt.Longopa amesema, anaamini sana katika ushirikiano na uhusiano mzuri miongoni mwa watumishi na kwamba, katika katika pindi chote ambachoKaimu Mkurugenzi alikuwa akiongozaIdara hiyo, Idara imetekeleza majukumu yake kwa uhodari wa hali ya juu na haikutetereka.

“Kwanza, nikupongeze Mkurungenzi (Kayichile) kwa kuteuliwa kushika nafasi hii ya uongozi,uongozi ni kupokezana kijiti, ni matumaini yangu kwamba Idara itaendelea kutekeleza majukumu yake vizuri ili hatimaye Idara ifikie malengo yake, na zaidi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ifikie malengo yake” Akasisitiza DAG

Na kuongeza kuwa “ Ninachopenda kutilia mkazo ni juu ya suala la ushirikiano na uhusiano mzuri miongoni mwenu, katika Idara yako, lakini pia na watumishi wote katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali”.

DAG amempongeza Bi. Mwaikambo kwa utekelezaji na usimamizi mzuri wa Idara hiyo tangukuondoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo Bi. Evelyne Makala.

“Nikushukuru sana kwa namna ambavyo ulisimamia utendaji kazi wa Idara hii mara tu ulipoteuliwa kukaimu. Nikiri kwamba, umetekeleza majukumu yako vizuri na Idara haikuyumba walakutetereka” Amesema DAG

Kwa upande wakeMkurugenzi wa Idara hiyo, Bw. Francis Kayichile pamoja na kushukuru kwa kuaminiwa na kupewa kijiti hicho ameahidi kwamba Watumishi wa Idara yake wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi kwa kile alichosema Idara inawatumishi wazuri na wenye weledi mkubwa.

Aidha amemuhakikishia DAG kwamba, ahatakikisha ushirikianondani ya Idara na nje ya Idaraunaendelezwa na kuimarishwa kwa kile alichosema utekelezaji wa majukumuya Idara hiyounategemea piamchango waIdara na Vitengo vingine ndani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Makabidhiano hayo pia yalishuhudiwa na Mkurugenzi wa Idaraya Utawala na Raslimali watuBw. Jackson Nyamwihula.

Imetolewa na Kitengo

Cha Mawasiliano

16/12/2019