Habari

Imewekwa: Jan, 10 2020

WAJUMBE WA KAMATI YA UKAGUZI WAPATIWA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO

News Images

WAJUMBE WA KAMATI YA UKAGUZI WAPATIWA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Imeelezwa kwamba, Kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, inayo majukumu makubwa zaidi ya kupokea na kupitisha Taarifa za Mkaguzi wa Ndani.

Hayo baadhi ya masualayaliyodhihirishwa wakati wa mafunzo ya siku tatu, kwa wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi yaliyofanyika katikaOfisi ya Ipagala, Jijini Dodoma.

Mafunzo haya yameratibiwa naKitengo cha Ukaguzi wa Ndani, na watoa madawalitoka Wizara ya Fedha na Mipango,Ofisi ya Mkaguzi MKuu wa Ndani.

Hii ni mara ya kwanza kwa wajumbe wa watano waKamatihii,na ambao wengi wao ni wapya, kupatiwa mafunzo yaliyolenga kuwajegea uwezo ikiwa ni pamoja na kutambua ukubwa wa majukumu yao na nafasi yaokatika Taasisi.

Kwa mujibu waBw.Athanas Pius ambaye ni mmoja wa watoa mada katika mafunzo haya, anasema "Kamati yaUkaguzini zaidi yakuangalia masuala ya fedha, ninyi mnatakiwa kwenda mbali zaidi kwa kufanyia kazi masuala mtambuka yanayohusuTaasisiyakiwamomasuala ya raslimali watu, mali za Ofisina utendaji mzima wa Taasisi".

Anakwendambali zaidi kwa kusema, Kamati yaUkaguzi ni washauri kwa watendaji wakuu wa Taasisi. Na kwa sababu hiyo suala la ushirikiano na kufanya kazi kwa karibu baina ya Kamati na watendaji wakuu waTaasisi ni jambo la muhimu sana.

Kwa mujibu wa watoa mada, ili kamati iweze kutekeleza majukumu yake inapashwa pia kuwa pamoja na mambo mengine, mpangokazi, bajeti, kuzifahamu kanuni na miongozo ya utekelezaji wa majukumu yake.

"Kama Kamati, mnazo kanuni na miongozo ya utekelezaji wa majukumu yenu, lakini kikubwa lazima muwe na mahusiano mazuri na mamlaka zauteuzi au uongozi wa juu na hususani Afisa Masuhuli,kwa kuwa na vikao nao mara kwa mara ili kwa pamoja Taasisi iweze kusoga mbele".

Vile vile watoa mada hao wamesisitiza kwamba, Kamati ya Ukaguzi ni washauri na si watoa maamuzi.

Baadhi ya masuala ambayo yametiliwa mkazo katika mafunzo hayo ni pamoja na suala la uhuruna nafasi ya Mkaguzi waNdani katika utekelezaji wa majukumu yake, utunzaji wa siri, uadilifu na uaminifu.

Akizungumzia nafasi ya Mkaguzi wa Ndani katika Taasisi yoyote ile, Bw. Alphonce Muro amewaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa, Mkaguzi wa Ndani katika utekelezaji wa majukumu yake,anapashwa kuwa huru pasipo kuingiliwa kwa namna yoyote au kupangiwa nini afanye na nini asifanye.

"Mkaguzi wa Ndanilicha ya kwamba anatakiwa kuwa na sifa stahili kuwa mkaguzi wa ndani, lakini pia anatakiwa kufanya au kuteleza majukumu yake pasipo kuelekezwa wapi akauge au nini asikague na anao uhuru wakuitisha faili lolote lile.

"Ukaguzi ni suala mtambuka, mkaguzi wa ndani haishii kukagua matumia ya fedha tu,kukagua fedha ni sehemu tu ya ukaguzi anapashwa kwenda mbali zaidi ya masuala ya fedha.

Wawezeshaji hao wakasisitiza pia kwamba, mkaguzi wa ndani anapashwa kupewa ushirikiano kutoka menejiment kwa kuwajukumu lake kubwa ni kuisaidia taasisi ili iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Jambolingine lililosisitizwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba hoja zote zinazoibuliwa wakati wa ukaguzi zinapatiwa ufumbuzi wakati wa vikao vya ukaguzi na kujiepusha nahoja kujirudia rudia.

Aidha watoa mada hao walielezea kusikitishwa kwao na namna hojaza ukaguzi ambazo zinawasilishwa Bunge, zinavyojibiwa pasipokuwa na viwango wala maoni au majibukuridhisha nahivyo kuibua hoja juu ya hoja.

Wakasema tatizo hili lipo karibu katika Wizara ya Taasisi zote za Serikali.

"Moja ya kazi ya Kamati ya Ukaguzi na kwa kushirikiana naMenejimenti ni kuhakikisha kwamba, hoja zinazoibuliwa na wakaguzi zinapatiwa majibu yanayojitosheleza na yakina na ambayo yatapelekea hoja kufungwa"

Na kuongez, na kama hakuna majibu basi utataribuufikiwe wa kuwa na majadiliano nawakaguzi ili hatimaye hoja hiyo ifutwe au ifungwe ili kuepusha kuendelea kujirudiamwaka nenda mwaka rudi

Washiriki wa mafunzo hayo, karibu kila mmoja wao ameeleza ni kwa namna gani amenufaika nayo na kubwa zaidi kuhusunafasi zao na ukubwa wa majukumu yao kama Kamati ya Ukaguzi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndaniimeipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuandaa mafunzo hayo na kusisitiza kwamba, mafunzo ya mara kwa mara kwa watumishi yanawaongezea tija katika utekelezaji wa majukumu yao.

Wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali niBi. Nkuvililwa Simkanga, Dkt. Gift Kweka,Bw. Constatine Mashoko, Bw. Jackson Nyamwihula na Bw. Waziri Kipacha ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati.

Mafunzo haya pia yalihudhuriwa na wajumbe walioalikwa kutoka Uhasibu, Utawala, Manunuzi na Kitengo cha Mawasiliano.