Habari

Imewekwa: Jan, 06 2020

WATUMISHI OAG WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA VVU

News Images

WATUMISHI OAG WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA VVU

Na Mwandishi Maalum

Dodoma

Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo wamejitokeza kwa wingi kushirikimafunzo kuhusu virusi vya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi.

Mafunzo hayo ambayo yameendeshwa na mwezeshaji Dkt. George Matiko kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kufunguliwa naNaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evarisho Longopa yalihusisha pia zoezi la kupima kwa hiari.

Mafunzo hayo yaliyokuwa katika mtindo wa majadiliano pamoja na kutoa mifano hai,yaliwavutia na kuwachangamsha washiriki kiasi cha wengi wao kuuliza maswali na hatimaye kujitokeza na kwenda kupima afya zao kwa hiari.

Dkt. George Matiko, ambaye alionekana kuimudu vema mada yake, pamoja na kuhimiza umuhimu wa kila mtu kijijengea utaratibu wa kupima afya na pamoja na familia yake. Alisisitiza kila mtumishi kujiepusha na mazingira hatarishi ikiwamo ngono zembe ili kuepuka kuambukizwa au kuambukizavirusi vya ukimwi.

Mtaalamu huyo wa masuala ya afya, pamoja na kuzungumzia na kujadili kwa kina kuhusu maambukizi na ugonjwa wa ukimwi, pia alizungumzia kuhusu homa ya Ini ambayo amesema kwa sasa ugonjwa huu ni tishio kubwa la kiafya hapa nchini na kwamba ni ugonjwa usiokuwa na tiba.

Na kwasababu hiyo, ameshauri na kusisitizaIdara ya Utawala na Raslimali Watu, kufanya utaratibu ili watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waweze kupima na kupatiwachanjo ya homa ya ini.

Akasisitiza kuwa ugonjwa wa Ini unaua haraka sana kuliko hata Ukimwi.

Awali akifungua mafunzo hayo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa, ametilia mkazo sana kwa watumishikuzifahamuafya zao.

Akasema kama mtumishi hafamu hali ya afya yake au afya yake inakuwa na mgogoro basi hata utekelezaji wa majukumu yake unakuwa na shida.

“Niwashukuru watumishi wenzangu kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mafunzo haya. Mafunzo haya yatatupa mwanga na kutusaidia kuziweka afya zetu vizuri nahivyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu” akasema DAG.

Mafunzo haya yameratibiwa na Idara ya Utawala na Raslimali Watu ikiwa ni utekelezaji moja ya malengo ya Mpango Kazi ambao Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imejiwekea.