Habari

Imewekwa: Oct, 22 2021

WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI WAPIGWA MSASA KUHUSU MAADILI YA UTUMISHI NA RUSHWA

News Images

Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamekubushwa kuzingatia kanuni za maadili ya Utumishi wa Umma na pia kujiepusha na vitendo vya Rushwa.

Kauli hiyo imetolewa leo kwa nyakati tofauti na wataalamu Jane Mahundi na Tulibalo Minga kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. (TAKUKURU)

" Watumishi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kama ilivyo kwa watumishi wote wa umma mnanapashwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, na pia tujiepushe na vitendo vya rushwa ili kwa pamoja muweze kuleta mafanikio katika Taasisi yenu na maendeleo kwa taifa letu" akasema Bi. Jane Mahundi.

Naye Bi Tulibako Minga akizungumza kuhusu Rushwa alisema Watumishi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanapashwa kuwajibika na kujiepusha na mazingira ambayo yanaweza kuwasababishia kupokea rushwa.

Kwa upande wao Watumishi hao katika ujumla wao wamewashukuru wataalamu hao kwa kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kujiepusha na vitendo au mazingira yanayoashiria rushwa.

Watumishi waliohudhuria mafunzo hayo ambayo ni wa ngazi zote walipata nafasi ya kuulizwa maswali au kupata ufafanuzi na hata wao wenyewe kuchangia mawazo yao juu ya dhama nzima ya maadilia katika mahala pa kazi na viashiria vya rushwa na namba namna ya kukabiliana navyo.

Wakasema mafunzo hayo ya mara kwa mara ya kukumbushana wajibu wao ni muhimu kwani yatawaondolea kuchukulia mambo poa wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Idara ya Utawala na Raslimali Watu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kufanyika katka Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma