Habari

Imewekwa: Jul, 23 2019

WATUMISHI WA OAG WAASWA KUZINGATIA MPANGO KAZI

News Images

MKURUGENZI WA MIPANG0 ASISITIZA UMUHIMU WA KUZINGATIA MPANGO KAZI

Na Mwandishi Wetu, Ipagala

Wakati mwaka mpya wa Serikali (2019/2020) ukiwa umeanza , Mkurugenzi wa Mipango katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Nkuvililwa Simkanga, amewataka na kuwahimiza Wakuu wa Divisheni na Vitengo kuhakikisha wanazingatia Mpango Kazi ( Action Plan ) ya Taasisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ametoa wito huo leo (jumanne) katika kikao kazi cha kuwaelimisha na kuwa na uelewa wa pamoja kwa Watumishikutoka Ukaguzi wa Ndani, Uhasibu na Tehama, juu ya Mpango Kazi waOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mwaka 2019/2020.

Katika maelezo yake ya awali Mkurugenzi Simkanga, amesema ni wajibu wa kila mtumishi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuvifahamuvipaumbele na malengo ya utekelezaji wamajukumu yaTaasisi kupitia Mpango kazi huo.

"Kukutana kwetu leo, pamoja na mambo mengine,ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Swerikali Profesa Adelardus Kilangi, ambaye ametutaka Idara yaMipango kutenga muda wa kukutanana Wakuu wa Idara, Vitengo na Watumishi walio chini yao kwa madhumuni yakuelimishanajuu ya Mpango Kazi (Action Plan ) ya mwaka huu wa fedha 2019/2020" akasema Mkurugenzi.

Akaongeza kwamba watumishi wote katika umoja wetutukiwa na uelewa wa mpango kazi wa taasisi yetu natukaumiliki, utatuwezeshasiyo tu kutekeleza vema majumuku tuliyojiwekealakini pia utatusaidia sana katika uaandaji wa taarifa zetu za robo mwaka na ujazaji wa fomu za Opras.

Mkurugenzi huyo wa Mipango, amewataka Wakuu wa Divisheni na Vitengo na watumishi wote kuondokana na dhana iliyojengekea miongoni mwao kwamba, mpango kazi wa Taasisihuwautekelezeki au haufuatwi.

"Ninawaomba sana tuondoe dhana hii ambayo imejengekamiongoni mwetu, kwambampango kazi wa Ofisihautekelezeki au haufuatwi wakati wautekelezaji wa majukumu yetu. Hii si sahihi,mpango kaziunatekelezeka ilimradi tuzingatie mwongozo wabajeti na vipaumbele ambavyo tumejiwekea sisi wenyewe" Amesisiza Mkurugenzi.

Ameongeza kwamba, kwa kila Mkuu wa Divisheni na Kitengo kuzingatia mwongozo wa bajeti na mgao wa fedha utakaokuwa unatengwa kutasaidia sana katika kuhakikishautekelezaji sahihi na wenye tija wamalengo ambayo kilaIdara na Kitengo imejiwekea na hivyo kutoyumbisha Bajeti ya Taasisi na pia itapunguza kulaumiana.

Mkurugenzi ametilia mkazo sana juu ya umuhimu wa kutekeleza majukumu yale ambayo yametengewa fedha hata kama itakuwa kidogo, na kwamba, kwa mwaka huu wa fedha mkazo na mgao wa fedha utaelekezwa kwenye malengo ambayo kilaIdara na Kitengo imejipangia.

Hata hivyo akasema, kama ilivyo kwa Taasisi nyingine, panaweza pakajitokeza majukumu ambayoyapo nje ya Bajeti na Mpango Kazi. Endapo itatokea hivyo basi hatua muafaka zitachukuliwa kwa namna itakayopaswa kuyashughulikiwa.

Katika hatua nyingine Mkurungezi waMipango amewataka Watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuifahamu kwa kichwa Dira na Dhima ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Huku akisisitiza kwamba ni aibu kwa mtumishi kutojua au kufahamuDira na Dhima ya Taasisi yake.

Idara ya Mipango umejipangia ratiba ya kukutana na kuelimishana kuhusu MpangoKazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu unauhusu pia Bajeti nzima iliyopitishwa na Bunge na mgawanyo wa Bajeti hiyo kwa kuzingatia vipaubele vya kila Idara na divisheni.

Katika Mwaka huu wa Fedha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepewaBajetiyaShilingiBilioni6,632,301,000. Kati ya hizo Mishahara nibilioni 3,013,570,000 na Matumizi mengineyo nibilioni 3, 618,731,000.