Habari

Imewekwa: Dec, 07 2021

WATUMISHI WENGI WAJITOKEZA KUPIMA AFYA ZAO NA KUPATA CHANJO

News Images

WATUMISHIWENGIWAJITOKEZA KUPIMA AFYA ZAO NA KUPATA CHANJO

NaMwandishi Maalum

Idadi kubwa ya watumishi wa kada mbalimbali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, waliopo Jijini Dodoma wameshiriki na kuhudhuria mafunzo kuhusu Homa ya INI ( Hepatitis,) magonjwa sugu yasiyoambukiza yakiwamo ya kisukari na shinikizo la damu.

Watumishi66 walihudhuria mafunzo hayo na kati ya hao, 49 walijitokeza kwahiariyao kupima afya zao.Kati ya 49 waliopima, 39 walikwenda kupata chanjo zilizotolewa na wataalamu wa Afya kutoka Hospitali ya Rufaa yaMkoani Ddodoma.

Mwitikio wa kupima na hatimaye kupata chanjo ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza ulikuwa ni mkubwa kiasi kwamba watumishi walikuwa wakihamasishana wao kwa wao pasi nashaka.

“Umeshapia,umeshachanja, mimitayari wewe je?” huku wengine wakionyeshavyeti vyao ndizo kauli zilizotawaka katikachumba cha mafunzo na hata katikakorido zaOfisi.

Awaliakifungua mafunzo hayo, Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bw. Said Nzori aliwahimiza watumishi waliohudhuria mafunzo hayo kwambakila mtumishianayo hiari yakufahamu afya yake kwa kupima na kupata chanjo.

Bw. Nzori amesema kupitia mafunzo hayo watumishi watapewa elimukuhusu ugonjwa wa Homa INI, Uviko 19, upimaji wa hiari wa Virusi vya ukimwi nakuchanja kwa watumishi watakao hiari ili kuwawezeshawatumishi kujikinga na kuchukua tahadhari kwa ajili yakulinda afya zao, familia zao namiongoni mwa watumishi.

“ Hivyo natoa wito kwa watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujenga utamaduni wa kupima afya zetu na pia kuchukuatahadhari juu yamagonjwa hayaikiwa nipamoja na kufanya mazoezi.” Akasisitiza Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu Bw. Nzori

Na Kuongeza “ Ninawaomba pia kupitia mafunzo haya mtakayopata mkaweze kuwa mabalozi kwa watumishi wenzetu ambao leo hajawaweza kupata mafunzo hayo. Ni matumaini yangu kuwamtakuwa makini, kusikiliza na kuyafuatilia mafunzo haya muhimu.”.

Wakati wa mafunzo hayo watumishi walipata fursa ya kuuliza maswalimbalimbali.

Elimu hiyo ya Afyakwa watumishi waOfisi ya Mwanasheria MkuuDodomaimetolewa naWataalamu wa Afya wakiwamomadaktari wawili ,manesi, wataalamu wa maabara nawafamasia kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Chanjoya Homa ya Ini iliyotolewa kwa hiari kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikalimjini Dodoma, imegharimiwa na Ofisi ambapo Idara yaUtawalana RaslimaliWatu ndiyo iliyoratibu mafunzo hayo kupitizia Mpangokazi wa Idara hiyo wa mwaka 2021/2022.

Serikali kupitia Ofisi yaRais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilitoa Waraka wa UtumihsiNa.2 waMwaka 2014 kuhusu kudhibiti virusi vya Ukimwi,Ukimwi na Magonjwa sugu yasiyoambukiza mahalapa kazi katika Utumishi wa Umma.