Habari

Imewekwa: Jul, 26 2019

YALIYOJIRI WAKATI WA KIAKO CHA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI

News Images

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUSHIRIKISHANA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI

 • Leo ilikuwa ni zamu ya Watumishi wa Idara ya Mikataba kujengewa uelewa waMpango Kazi wa mwaka wa fedha 2019/2020
 • Jambo la muhimulililojitokeza wakati wa kikao hicho, pamoja na mambo mengine, ni haja na umuhimukwa Wakuu wa Idara na Vitengo na watumishi wote kwa ujumla kujiwekea mkakati wa makusudi kabisa wa kuboresha taarifa za utekelezaji za kila robo ya mwaka.
 • Azimio hilo linatokana na ukweli kwamba, baada yawatumishi kupitishwa kuhusu Mpango Kazi huo na bajeti ambayo Taasisi imetengewa kwa mwaka huu wa fedha, kubaini kwamba, ukilinganisha na majukumu makubwa, mazito na nyetiyanayotekelezwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalihayaendani na bajeti iliyotengwa.
 • Imebainishwa kwamba moja ya changamoto zinazopelekeaTaasisi kutopata bajeti inayokidhi mahitaji ya Ofisi ni kutokuwapo na taarifa sahihi na zilizoshehenitakwimu namaelezo yanye kutafasiri takwimu hizo.
 • Akichangia majadiliano hayo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba na Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia Sehemu ya Mikataba ya Kimataifa, Bw. Francis Kayichile
 • Akasema “ Hapa hakuna cha kujitetea, tunatakiwa kubadirika na kujipanga vizuri, ni kweli tunafanya kazi kubwa ya upekuzi wa mikataba mikubwa, mizito na nyeti tunafanya kazi kwa masaa mengi, tunapashwa kuzirekebisha taarifa zetu za utekelezaji kwa kuziboresha na kuzifanya zionyesheuhalisia wa utekelezaji wa majukumu yetu na ya Taasisi nzima”. Akasema Mkurugenzi Msaidizi.
 • “Akaongeza kwamba, pamoja na changamoto mbalimbali zikiwamo za uchache wa watumishi, lakini bado hao wachache waliopo wanategemewa na nchi nzima. Na tumeanza utaratibu wa kila mtumishi anayekwenda kufanya kazi fulani nje ya Ofisi lazima aandike taarifa . Tumeanzisha huu utaratibu “ Back to OfficeReport” hii itasaidia sana katika uandikaji wa taarifa zetu na hivyo kuwa na tija zaidi”.
 • Awali Mkurugenzi wa Mipango, Bibi Nkuvililwa Simkaga akieleza madhumuni ya ushirikishwa wa watumishi juu ya mpango kaziwa ofisikwamba ni maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Profesa Adelardus Kilangi.
 • Akatilia mkazo kwa kusema kwamba, Idara za Kisheria ndizo zinazobeba Taswira ya Ofisi na zinafanyaau zinatekeleza majukumu makubwa na mengi lakini taarifa zake ni taabu sana kupatikana na hata zikipatika basi ni kwa kuchelewa na hazibebi sura halisi ya kazi zilizotekelezwa.
 • “Nawaomba sana sana Idara za Kisheria ndizo zinazobeba Bajeti ya Taasisi hii, lakini kuna mahali tunakwama nako ni kwenye taarifa zilizosheheni Takwimu na zenye maelezo ya kina. Tukiboresha taarifa zetu zitatusaidia sana sana. Na niomba mwaka huu tuanze mapema katika maandalizi yataarifa zetu taarifa zetu zizungumze. Tusiangushane sote tutimize wajibu wetu ili tuondoke hapa tulipo”. Akasisitiza Mkurugenzi.
 • Katika mwaka huu wa fedha 2019/2020 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetengewa Tsh. 6,632,301,000 kati ya hizo Tshs. 3,013,570,000 ni kwa matumizi ya mishahara na Tshs.3,013,579,000 ni kwaajili ya matumizi mengineyo.