Mikataba na Makubaliano
Divisheni hii ni moja ya Divisheni Tatu (3) za Kisheria katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kazi zake za msingi ni kutoa ushauri na kuendesha majadiliano kwa niaba ya Serikali katika Mikataba yote. Idara inaongozwa na Mkurugenzi pamoja na Wakurugenzi wasaidizi.
Majukumu ya Divisheni ya Mikataba
- Uhakiki wa Mikataba ya Manunuz.i
- Uhakiki wa Makubaliano ya Kitaifa na Kimataifa.
- Kuhudhuria na kutoa mapendekezo ya Nchi katika Vikao vya Kikanda na Kimataifa kwa maslahi ya Nchi.
- Kuhudhuria Vikao vya Majadiliano ya Mikataba mbalimbali yenye maslahi kwa nchi kila inapohitajika.
- Kutoa Ushuri kwenye Mikataba ya Mikopo.
Sehemu za Divisheni ya Mikataba
Divisheni hii ina Sehemu Tatu (3) zinazoongozwa na Wakurugenzi Wasaidizi. Sehemu hizo ni :-
- Sehemu ya Mikataba ya Ununuzi wa Umma
- Sehemu ya Mikataba ya Makubaliano ya Kimataifa
- Sehemu ya Mikataba ya Uwekezaji, Maliasili na Fedha.