Uratibu na Ushauri wa Kisheria
Hii ni Divisheni ya Tatu ya Kisheria Katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Divisheni hii inahusika na Utoaji wa Ushauri wa Kisheria kwa Wizara, Divisheni zinazojitegemea, Wakala, Taasisi za Serikali na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Divisheni inaongozwa na Mkurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi.
Majukumu ya Divisheni ya Uratibu na Huduma za Ushauri
- Kitoa Ushauri wa Kisheria kwa Wizara na Taasisi za Serikali
- Kuratibu masuala yote ya sheria katika Taasisi za Serikali na kutoa mrejesho
- Kuhudhuria Vikao vya Kikanda na Kimataida kila inapohitajika
- Kuhudhuria Vikao cha Majadiliano ya Mikataba mbalimbali yenye maslahi kwa nchi hii inapohitajika.
Sehemu za Divisheni ya Uratibu na Huduma za Kisheria
- Sehemu ya Majadiliano na Usimamizi wa Mikataba
- Sehemu ya Uratibu
- Sehemu ya Ushauri wa Kisheria