Kuanzishwa

Ofisi ya Mwanashera Mkuu wa Serikali ni Taasisi inayojitegemea ndani ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mujibu wa Kanuni Na. B.2 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la 2009. Ofisi imeanzishwa chini ya Ibara ya 59 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yamwaka 1977 pamoja na Sheria yaUtekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sheria Na.4 ya Mwaka 2005. Jukumu la msingi la Ofis hii nikuishauri Serikali kuhusu mambo yote muhimu ya kisheria kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 59 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanasimamiwa na Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura ya 268 na Muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Majukumu ya Msingi

Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 48 la mwaka 2018 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ina majukumu yafuatayo;-

i.Kuishauri Serikali katika masuala ya Mikataba na uandishi wa sheria;

ii.Kuratibu na kutoa ushauri wa kisheria;

iii.Kuendesha majadiliano kwa niaba ya Serikali katika Mikataba yote;

iv.Kupitia mikataba ya kibiashara na ya kimataifa kwa niaba ya Serikali na kuishauri Serikali ipasavyo

v.Kusimamia wajibu wa kimikataba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

vi.Kuandaa miswada ya sheria ya kupitishwa Bungeni;

vii.Kuandaa hati zote za kisheria na maazimio kwa ajili ya kuidhinishwa na Bunge;

viii.Kushauri Wizara, Idara za Serikali na taasisi nyingine za Serikali;

ix.Kushiriki katika kudhibiti nidhamu ya Mawakili wa Kujigetemea kupitia Kamati ya Maadili ya Mawakili ( Advocates Committee);

x.Kuendesha na kusimamia mafunzo kwa njia ya vitendo kwa wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwavitendo;

xi.Kuwasimamia Maafisa Sheria na Mawakili wa Serikali wote walioko katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali katika kutekeleza majukumu yao ya kisheria;

xii.Kushauri kuhusu Sera za Nchi kuhusiana na usimamizi wa utawala wa Sheria Tanzania pamoja na kusimamia taaluma ya Sheria;

xiii.Kutoa ushauri kuhusiana na Nyaraka za Baraza la Mawaziri (cabinet papers), memoranda na ufuatiliaji wa ahadi za utekelezaji wa maamuziyanayohitaji kutungwa kwa sheria ama kuundwa chombo chochote cha kisheria; na

xiv.Kutekeleza jukumu lolote linaloweza kuwa muhimu kwa utekelezaji ulio na ufanisi wa majukumu na utekelezaji wa mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Aidha Majukumu ya Ofisi yanasimamiwa na kuongozwa na sheria mbalimbabli zikiwamo

i. Sheria ya Mwenendo wa Mashauri dhidi ya Serikali (The Government Prosecuting Act) (Cap 5);

(ii) Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Sura 20);

iii. Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai (Sura 33);

iv. Sheria ya Kanuni za Adhabu (Sura 16);

v. Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (The Basic Rights and Duties Enforcement Act)(Cap 3);

vi. Sheria ya Tafsiri ya Sheria (The Interpretation of Laws Act)(Cap 1);

vii. Sheria ya Mahusiano ya Kusaidiana katika Masuala ya Jinai (The Mutual Assistance in Criminal Matters) (Cap 254);

x. Sheria ya Urejeshwaji wa Watuhumiwa katika Nchi waliyofanya Kosa (The Extradition Act) (Cap 368); na

ix. Sheria ya Ubia Baina ya Umma na Watu Binafsi (The Public Private Parthership Act) (Cap 103).