OUR HISTORY
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanzishwa chini ya Ibara ya 59 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Jukumu kubwa la Ofisi hii ni kuishauri Serikali katika masuala yote ya kisheria ndani na nje ya Nchi katika maeneo yote ya Uandishi wa Sheria, Urekebu wa Sheria, Ufasiri Sheria, Upekuzi na Uchambuzi wa Mikataba mbalimbali ya kiuwekezaji. Aidha, Ofisi hi inaiwakilisha Serikali Kitaifa, Kikanda na Kimataifa katka masuala yenye maslahi kwa Taifa kama yalivyoonneshwa katika Ibara ya 59(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na katika Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Sura ya 260.