Uandishi wa Sheria
Divisheni hii ni kati ya Divisheni Tatu za Kisheria katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kazi za msingi za Divisheni hii ni kuandaa na kuandika Miswaada ya Sheria zote zinazotungwa na Bunge na Sheria ndogo zinazotungwa na Mamlaka mbalimbali. Divisheni pia inahuka na kutafsiri sheria kutoka lugha ya Lugha ya Kiingereza kwenda Lugha ya Kiswahili. Divisheni hii pia inalojukumu la kufanya urekebu wa sheria zote za nchi. Idara inaongozwa na Mkurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi.
Majukumu ya Divisheni ya Uandishi wa Sheria
- Uandaaji wa Miswaada ya Uandishi wa Sheria
- Tafsiri ya Sheria kutoka lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili
- Urekebu wa Sheria
- Kuhudhuria Vikao vya Kikanda na Kimataifa vinavyohusu uandishi wa Sheria kila inapohitajika na kutoa ushauri wa Kisheria.
Sehemu za Divisheni ya Uandishi wa Sheria
- Sehemu ya Uandishi wa Sheria
- Sehemu ya Urekebu wa Sheria
- Sehemu ya Fasiri ya Sheria