Ushauri wa Kisheria

Ushauri wa Kisheria

 

  1. Kuishauri Serikali  juu ya masuala yote  ya kisheria ikiwemo Mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania ni sehemu ya Mkataba ama ina maslahi katika Mkataba hiyo;
  2. Kushauri na kudumisha uhusiano kati ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa lengo la kuleta ufanisi  katika suala lolote lililopo Mahakamani na katika Mabaraza;
  3. Kupokea  taarifa kutoka kwa Wakili Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Mashtaka kwa dhumuni la kuishauri Serikali, Bunge na Mahakama;
  4. Kuwasimamia Maafisa Sheria na Mawakili wa Serikali wote walioko katika Wizara, Idara na Taasisi za Seriakli  katika  kutekeleza majukumu yao ya kisheria;
  5. Kushiriki katika kudhibiti nidhamu ya Mawakili wa Kujitegemea kupitia Kamati ya Maadili ya Mwakili; na  Kutekeleza jukumu  lolote linaloweza kuwa muhimu kwa utekelezaji ulio na ufanisi wa majukumu na mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.