MAKALA MAALUM YA MKUTANO WA MAWAKILI WA SERIKALI ULIOFANYIKA TAREHE 29/09/2022 DODOMA

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria iliandaa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mawakili wa Serilaki uliofanyika tarehe 29/09/2022 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Dodoma. Mgeni Rasmi katika Mkutano huo alikua ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pamoja na maswala mengine alizindua Chama cha Mawakili wa Serikali, Mfumo wa OAGMIS pamoja na nembo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hii ni makala maalum ya mkutano huo mkubwa.